August 15, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Simba kumekucha, Okrah kuungana na Chama, Sakho safarini Misri kesho

Spread the love

 

KLABU ya Simba imeendelea kushika kasi kwenye usajili wa wachezaji mbalimbali, kufuatia hii leo tarehe 13 Julai 2022, kutmabulisha kiungop mshambuliaji Agustine Okrah raia wa Ghana. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Mchezaji ametambulishwa hii leo na uongozi wa klabu hiyo, kufuatia kukamlika kwa mazungumzo ambayo yalianza muda mrefu kati ya klabu na mchezaji huyo.

Okrah atakuwa sehemu ya kikosi cha Simba kitakacho paa kesho kuelekea nchini Misri kwenye mji wa Ismailia, tayari kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa mshindano 2022/23.

Tayari wachezaji wengine wa klabu ya Simba kama vile Clatous Chama pamoja na Pape Ousmane Sakho tayari wameshawasili nchini kwa ajili ya safari hiyo ya kesho nchini Misri.

Katika msafara huo baadhi ya wachezaji ambao watajumuishwa kwenye na kocha Kim Poulsen kwenye kikosi cha Timu ya taifa ya Tanzania “Taofa Stars”, hawatokuwa sehemu ya safari hiyo kufuatia kuwa na mchezo wa kimataifa dhidi ya Somalia.

Klabu hiyo inasafiri huku bado ikiwa haijamaliza kutambulisha wachezaji wake wapya hasa wa kimataifa, mara baada ya kusema kuwa wameshamaliza kusajili wachezaji wa ndani.

Simba itaakaa nchini Misri kwa siku 14 sawa na wiki mbili, kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao ambao watakuwa na kibarua kingine cha kuiwakilisha nchi kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

error: Content is protected !!