Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Wadau wataka sheria makosa mtandaoni iandikwe upya
Habari Mchanganyiko

Wadau wataka sheria makosa mtandaoni iandikwe upya

Waandishi wa Habari
Spread the love

 

WADAU wa tasnia ya habari nchini Tanzania, wameshauri Sheria ya Makosa ya Mtandaoni ya mwaka 2015, ifutwe ili kutoa nafasi ya kutungwa upya kwa lengo la kuondoa mapungufu yaliyokuwepo. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Wito huo umetolewa kwenye mkutano wa wahariri wa vyombo vya habari mbalimbali, uliosimamiwa na Jukwaa kwa Wahariri Tanzania (TEF), jana jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika mkutano huo, Mhariri wa Gazeti la Majira, Imma Mbuguni, alisema sheria inabidi iandikwe upya Kwa kuwa ilipitishwa kwa dharura bila muswada wake kujadiliwa na wadau kwa ajili ya kutoa mapendekezo ya kuiboresha zaidi.

“Sheria ya Makosa ya Mtandaoni ifutwe na mchakato wake uanze upya. Sheria hii pamoja na uzito wake, kwanza ilipitishwa kwa hati ya dharura lakini vifungu vyake vingi vinajikita katika dhana,” alisema Mbuguni.

Akizungumza katika mkutano huo, Wakili wa kujitegemea, James Marenga, alisema “Waandishi wanaweza kuweka shinikizo, Sheria ya Makosa ya Mtandaoni ikafanyiwa marekebisho upya. Vifungu vingi vinajiekeza kwenye dhana, na ni ngumu kuhakiki dhana mahakamani.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yazindua huduma maalum kwa wastaafu

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua huduma maalum kwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yazindua akaunti ya Kikundi

Spread the loveBenki ya NMB imezindua akaunti ya kikundi yenye  maboresho makubwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyakazi waidai STAMICO mishahara ya bilioni 1

Spread the loveWALIOKUWA wafanyakazi wa mgodi wa Shirika la Madini la Taifa...

AfyaHabari Mchanganyiko

200 wapimwa afya na GGML katika maonesho ya OSHA

Spread the loveZAIDI ya watu 200 jijini Arusha wamejitokeza kupimwa afya na...

error: Content is protected !!