Saturday , 20 April 2024
Home Habari Mchanganyiko VETA yarasimisha vijana 10,000
Habari Mchanganyiko

VETA yarasimisha vijana 10,000

Afisa uhusiano VETA, Dorah Tesha
Spread the love

 

MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) nchini Tanzania imetoa mafunzo na vyeti kwa vijana zaidi ya 10,000 nchi nzima wenye ujuzi nje ya mfumo rasmi wa kupitia mamlaka hiyo. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Hayo yamebainishwa na Afisa Uhusiano VETA, Dorah Tesha alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya mafunzo na mikakati inayofanywa na chuo hicho sambamba na kuwarasimisha vyeti vya ujuzi vijana ambao wamepata ujuzi nje ya mfumo rasmi.

Dorah akiwa katika maonesho ya elimu ya ufundi shindani yanayoratibiwa na (Nactvet) na kueleza kwa sasa vyuo vya VETA vimejengwa 40 nchi nzima na ujenzi wa vyuo kila wilaya unaendelea.

Aidha, amesema kutokana na vijana wengi kupata ujuzi mitaani bila kupitia vyuo vya VETA kwa kushirikiana na ofisi ya waziri mkuu walianzisha kitengo cha kupitia maeneo mbalimbali na kuweza kutoa elimu kwa vijana hao na kuwapatia vyeti vya ujuzi ili kuweza kuwafanya waweze kupata ajira za uhakika au kupata tenda kadri ya kile anachokijua.

“Serikali iliona wapo vijana wengi ambao wanaujuzi wa kufanya shughuli mbalimbali lakini hawana vyeti hivyo hawawezi kuomba kazi popote wakapata.”

“Kutokana na hali hiyo VETA kwa kushirikiana na ofisi ya waziri mkuu ilianzisha utaratibu wa kupita kwenye magereji pamoja na sehemu mbalimbali na kutoa mafunzo kwa vijana ambao wamekuwa na ujuzi nje ya mfumo rasmi kwa zaidi ya miaka mitano na kuwarasmisha vyeti vya ufundi,” amesema

“Kutokana na mkakati huo zaidi ya vijana 10,000 wamerasimishwa vyeti vya ujuzi kutoka VETA na kwa kufanya hivyo tayari vijana hao kwa sasa wanaweza kuajiriwa, kuomba zabuni yoyote kulingana na ujuzi wa mtu alionao,” amesema

Aidha, afisa huyo amesema nafasi za kuwapata mafunzo na vyeti vijana ambao wanaujuzi nje ya mfumo rasmi utolewa kila baada ya miezi mitatu na mafunzo hayo utolewa bure kwani ugharamiwa na serikali.

Pamoja na mambo mengine, Dorah amesema VETA itoa mafunzo ya aina yoyote ya ufundi ambayo umwezesha mtu yoyote kuweza kujiajiri au kuajiriwa na kueleza mafunzo hayo utolewa kwa muda mfupi na muda mrefu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

error: Content is protected !!