Tuesday , 30 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Bilioni 20 kufufua mashamba ya alizeti, michikichi
Habari Mchanganyiko

Bilioni 20 kufufua mashamba ya alizeti, michikichi

mazao la Alizeti
Spread the love

 

RAIS Samia Suluhu Hassan, amesema Serikali imetenga Sh. 20 bilioni kwa ajili ya kuyaendeleza mashamba makubwa, ikiwemo ya alizeti na michikichi, kwa ajili ya kuimarisha hali ya upatikanaji rasilimali za viwandani. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kagera…(endelea).

Rais Samia ameyasema hayo katika uzinduzi wa awamu ya tatu ya ujenzi wa mtambo wa kuzalisha umeme katika Kiwanda cha Sukari cha Kagera, uliofanyika leo Alhamisi, tarehe 9 Juni 2022.

Ris Samia amesema, Serikali yake imeanzisha sera ya kilimo cha mashamba makubwa, ambapo moja mkoa uliolengwa katika utekelezaji wa sera hiyo ni Kagera.

“Kagera mna ardhi nzuri kubwa, lakini haitumiki maeneo mengi yamebaki. Sasa tumekuja na sera ya kilimo cha mashamba makubwa. Moja ya mkoa tuliolenga kwa kilimo cha mashamba makubwa ni hapa Kagera. Serikali tumetenga bilioni 20 kuyaendeleaza mashamba,” amesema Rais Samia.

Rais Samia amesema, mazao yakatopewa kipaumbele katika mashamba hayo ni alizeti na michikichi, ili kuisaidia nchi kupata malighafi za kutengeneza mafuta ya kupikia kwa ajili ya kupunguza changamoto ya upungufu wake.

Aidha, Rais Samia amesema Serikali yake imedhamiria kufanya mageuzi katika sekta ya kilimo hasa kwenye mazao ya chakula, ili kuifanya Tanzania kuwa muuzaji wa bidhaa za kilimo duniani, miaka 50 ijayo.

“Ni vyema kila mmoja kutambua kwa miaka 50 ijayo biashara itategemea sana kilimo na hasa mazao ya chakula dunia nzima. Hivyo haruna budi kuifanya nchi yetu kuwa mzalishaji mkubwa wa bidhaa za kilimo na hivyo kuwa ncho bora ya kuuza nje bidhaa hizo,”a mesema Rais Samia na kuongeza:

“Kwa muktadha huo ni wajibu wetu tukafanye mageuzi ya kilimo ambayo yataenda sambamba na ukuzaji wa viwanda hususan vile vinavyotumia malighafi za kilimo.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Oryx gesi yagawa mitungi, majiko 100 kwa waandishi wa habari Dar

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gesi Tanzania imegawa mitungi 100 ya gesi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

Habari Mchanganyiko

TMA yapongezwa kuimarisha ubora na usahihi wa taarifa za Hali ya Hewa

Spread the love  WAFANYAKAZI wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA),...

error: Content is protected !!