August 15, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mwakalebela akubali yaishe, atangaza rasmi kutogombea kwenye uchaguzi mkuu

Spread the love

 

MWANACHAMA mwandamizi na makamu mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Frederick Mwakalebela ameweka wazi nia yake ya kutogombea nafasi yoyote ya uongozi ndani ya klabu hiyo, kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika tarehe 10 julai 2022. Anaripoti Kelvin Mwaipungu….(endelea)

Kiongozi huyo wa sasa wa Yanga, ameyasema hayo hii leo tarehe 9 Juni 2022, kwenye makao makuuu ya klabu hiyo, nakuweka wazi nia yake ya kuunga mkono Mhandisi Hersi Said ambaye amerejesha fomu ya nafasi ya Urai ndani ya klabu hiyo.

Mwakalebela alisema kuwa, dhamira yake kwa sasa sio kuchukua fomu kwenye uchaguzi huu wa siku za hivi karibuni, na kukili kuwa mafanikio yote wanayopata klabu hiyo kwa sasa, hawakuwa peke yao bali kuna baadhi ya watu waliwaunga mkono

“Mimi dhamira yangu haikuwa kuchukua fomu kwa msimu huu, tumeona jinsi tulivyopipokea timu katika kipindi kigumu na tumefika kipindi cha neema, hatuwezi kusema tumefika hapa peke yetu, kuna watu walikuwa nyuma kusaidia kufika pale.” Alisema Mwakalebela

Aidha kiongozi huyo mwandamizi aliendelea kusema kuwa, aliamua kuja klabuni hapo siku ya leo, ili kuwaaga rasmi wanachama na mashabiki wa timu hiyo kwa kuwa hatogombea tena kwenye uchaguzi huu, bali kwa sasa ataunga mkono jitihada za mhandisi Hersi Said ambayo amerudisha fomu ya nafasi ya urais.

“Mimi nimekuja kuaaga rasmi mashabki wa Yanga kwamba sitagombea na kuUnga mkono jitihada za Hersi kugombea urais kwa klabu yetu ya Yanga.” Alisitiza kiongozi huyo

Hersi alichukua fomu kimya kimya siku za hivi karibuni mara baada ya utaratibu huo kutangazwa na Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya klabu hiyo Wakili Mchungahela, na siku ya leo alirejesha fomu hiyo huku akisindikizwa na baadhi ya wanachama wa klabu hiyo.

Yanga inakwenda kufanya uchaguzi huo kwa mara ya kwanza, toka walipofanya mabadiliko ya katiba na hivyo cheo cha Mwenyekiti wa klabu hiyo kwa sasa nkitfahamika kama rais wa klabu.

error: Content is protected !!