Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Mtaka aanika madhaifu wakandarasi wa ndani
Habari Mchanganyiko

Mtaka aanika madhaifu wakandarasi wa ndani

Spread the love

WAKATI wahandisi na wakandarasi wa ndani wakimpongeza Rais Samia kwa mchango wake kuimarisha wakandarasi wa ndani, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka ametaka pongezi hizo ziende na uwajibikaji wao katika utekelezaji wa miradi. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Mkuu huyo wa mkoa ameelezea madhaifu kadhaa ya wakandarasi wa ndani pindi tu wanapopewa miradi ya kutekeleza ikiwemo kushindwa kumalizia miradi.

“Pongezi nzuri kwa rais ni kazi yenu kuwa nzuri,” amesema Mtaka leo Jumamosi tarehe 4 Juni, 2022 kwenye kongamono la pongezi kwa Rais lililofanyika jijini Dodoma.

“Naomba sana hii tuibebe ili hawa vijana wanaomaliza shule wawe na tamaa ya kuja kuanzisha kampuni za ukandarasi lakini kama wanaona tunavyofukuzana hawezi kuhamasika.

Mtaka amesema kutofanya vizuri kwa wakandarasi wa ndani kumewasababishia matatizo watumishi wa Serikali kuonekana wanatoa kazi kwa kuhongwa.

“Tunapofanya pongezi ni vizuri taasisi za ukandarasi zibebe commitment kesho tusiende kufukuzana kwenye kazi, kuharibiana kazi tusifike mahali mtu akatamani hata kazi ya kilomita mbili ampe mchina kwasababu mmeleta matatizo mengi kwa watumishi wa Serikali kwa kuonekana wamewapa kazi kwa kuhongwa.

“Mtumishi anakuwa very genuine, unaenda mwenyewe TANePs unaomba kazi unapewa, ukiharibu sisi viongozi tunakuja tunamwadhibu waliokupa kazi na public inasema wote wamehongwa kuanzia meneja wa manunuzi, tunaharibu heshima ya watumishi wetu kwa ninyi wenyewe wakandarasi wenu kuwa na madeni mengi wanaharibu kazi na sisi tunaonekana wa hovyo kwasababu ya kuwapa kazi,” amesema Mtaka.

“Wakandarasi wa ndani wanaaminika wanapewa kazi anakuja na tenda na anaonesha umahiri wake, mpe kazi, mpe hiyo kazi, kesho kazi aliyoomba mwenyewe unaenda na Takukuru unaenda na Polisi, kuna watu wamemalizia kazi wakitokea ‘lock up’ kwenda kumalizia kazi.

Amsema wapo watumishi wameadhibiwa kwa kudhani wamehongwa na mkandarasi, “mkandarasi kapewa ‘advance payment’ kuna madeni anadaiwa Lindi anaenda kulipa madeni Lindi. Tunakuja kwenye ‘partnership’ wakilipwa tu ‘partnership’ imevunjia kila mmoja kivyake tumeharibu sana heshima ya taasisi zetu TARURA, TANROADS kazi ni kufukuza wandarasi wa ndani.”

“Tunawapa maneno wakandarasi wa nje, wanatuambia kweli mmesema chini ya kilomita 10 mnapeana wenyewe Watanzania sasa yako wapi, mmepeana mmeishia kufukuzana kuna makampuni hayaamini tena hata benki,” amesema Mtaka.

“Tuibebe hii commitment tumwahidi Rais kuwa kwenye bajeti yake ijayo hakuna mkandarasi ataharibu kazi,” amesema.

1 Comment

  • Kwa nini hakuna “standard quality and cost” ya ujenzi wa lami kilometa moja. Lazima hii standard iwepo na kufuatia hapo ni “bei” ya ujenzi haiwezi kuzidi 15% ya gharama halisi. Tuache kubembelezana.
    Atakayeshindwa kujenga kwa bei na wakati sahihi afutiwe leseni na asiruhusiwe kufanya ukandrasi tena.
    Nchi zote zilizoendelea zimepita huko. Asiyetaka kufanya kwa ufanisi na ubora ASIPEWE.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yazindua huduma maalum kwa wastaafu

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua huduma maalum kwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yazindua akaunti ya Kikundi

Spread the loveBenki ya NMB imezindua akaunti ya kikundi yenye  maboresho makubwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyakazi waidai STAMICO mishahara ya bilioni 1

Spread the loveWALIOKUWA wafanyakazi wa mgodi wa Shirika la Madini la Taifa...

AfyaHabari Mchanganyiko

200 wapimwa afya na GGML katika maonesho ya OSHA

Spread the loveZAIDI ya watu 200 jijini Arusha wamejitokeza kupimwa afya na...

error: Content is protected !!