Tuesday , 16 April 2024
Home Gazeti Habari Uchebe azua hofu kurejea Simba, alia upweke
HabariMichezo

Uchebe azua hofu kurejea Simba, alia upweke

Spread the love

KOCHA mkuu wa klabu ya AFC Leopards inayoshiriki Ligi Kuu nchini Kenya, Patrick Aussems maarufu kama ‘Uchebe’ ameondoka nchini humo kabla ya msimu wa ligi kukamilika. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Kocha huyo wa zamani wa Simba SC. Amezua hofu kwa mashabiki wa timu hiyo kwamba huenda amekwenda kuweka mipango ya kurejea Tanzania hasa ikizingatiwa Wekundu hao wa Msimbazi wamemtimua kocha Mkuu, Pablo Martin.

Aidha, kupitia mtandao wa Twitter, jana tarehe 3 Juni, 2022 Aussems amesema kuwa ni wakati wa kufurahia likizo na familia yake baada ya kuishi kwa upweke nchini Kenya tangu msimu ulipoanza mwaka jana.

Katika picha za tiketi yake ya ndege alizozibandika kwenye mitandao, Aussems hajaelekea nyumbani kwake Ubelgiji bali ameelekea Marseille nchini Ufaransa kupitia Addis Ababa, Ethiopia.

“Kwaheri Nairobi! Baada ya miezi minane ya kuishi pekee yangu, ni wakati wa kufurahia na familia yangu. Mke wangu na watoto wangu wavulana waliorejea kutoka Canada ili kuwa na sisi kwa siku kadhaa,” Aussems aliandika.

Kocha huyo aliyejipakulia jina la Uchebe kutoka mitaa ya Msimbazi, ameondoka nchini Kenya huku AFC Leopards ikiwa na mechi mbili za kucheza kukamilisha msimu. Kocha msaidizi Tom Juma ametwikwa majukumu ya kunoa timu hiyo kwa mechi zilizosalia.

Aidha, Aussems amewahakikishia mashabiki wa timu hiyo kuwa atarejea kuendeleza kazi yake msimu ujao.

“Mashabiki, wafanyakazi na wachezaji wa AFC Leopards ‘Ingwe’ malizeni mechi mbili zilizobaki katika sehemu ya kazi nzuri ambayo tumefanya kufikia sasa. Tutaonana hivi karibuni,” Aussems aliongeza.

AFC Leopards inashika nafasi ya sita kwa kuwa na alama 45 kwenye msimamo wa ligi hiyo huku ikiwa imebaki na mechi dhidi ya Nairobi City Stars (tarehe 5 Juni) na Nzoia Sugar (tarehe 11 Juni) kufunga msimu.

Aussems ameondoka baada ya kupoteza kombe la Madaraka kwa watani wao wa jadi Gor Mahia kupitia mikwaju ya penalti baada ya sare ya 1-1.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Leo ni leo nani kutinga nusu fainali UEFA?

Spread the love HATIMAYE Jumanne ya UEFA imefika ambapo leo hii michezo...

Michezo

Anza Jumatatu yako na Meridianbet

Spread the love  IKIWA ni siku nyingine mpya kabisa ya Jumatatu baadhi...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC, Yanga wazindua kadi  za kimataifa za uanachama

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kushirikiana na Klabu...

Michezo

TFF, Amrouche ngoma nzito

Spread the loveVIPENGELE vya mkataba wa kazi aliotia saini Kocha Mkuu wa...

error: Content is protected !!