Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Wasomi Marekani watua nchini kujifunza mabadiliko tabianchi
Habari Mchanganyiko

Wasomi Marekani watua nchini kujifunza mabadiliko tabianchi

Mkurugenzi wa Menejimenti ya Maarifa kutoka Costech Samson Mwela
Spread the love

Wasomi Marekani watua nchini kujifunza mabadiliko tabianchi

WASOMI kutoka chuo cha Northeastern kilichopo katika mji wa Boston nchini Marekani wametua nchini kupitia Tume ya Taifa ya Sayansi (COSTECH) kwa lengo la kujifunza na kubadilishana uzoefu juu ya kukabiliana na mabaliko ya tabia ya nchi. Anaripoti Faki Ubwa … (endelea).

Akizungumza na waandishi wa Habari kwenye Kongamano la kubadilishana uzoefu leo tarehe 1 Juni, 2022 Mkurugenzi wa Menejimenti ya Maarifa kutoka Costech Samson Mwela amesema ujumbe huo ni wa watu 35.

Mwela ameongeza kuwa dhamira ya msafara huo ni kubadilishana uzoefu kwenye utafiti na sayansi.

“Wamekuja kukutana na watafiti wenzao kwani kila nchi ina mikakati yake na sera zake kwa hiyo wenzetu wamekuja kujifunza kuhusu sera zetu hasa zinazotokana na tafiti za kisayansi,” amesema Mwela.

Amesema kuwa Costech ndio mtatibu mkuu wa masuala ya utafiti na sayansi pia ina jukumu la kujenga mahusiano kama ambavyo nchi yetu ipo kwenye kuutangaza utalii.

Aidha, Mhadhiri kutoka Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili (Muhas), Dk. Khadija Malima amesema pamoja na mambo mengine katika mkutano huo watafiti hao watabadilishana uzoefu kwenye mabadiliko ya hali ya nchi yanavyoathiri afya ya binadam.

“Mabadiliko ya hali ya nchi yanahusiana na afya ya binadamu, magonjwa ya mlipuko yanaongezeka kila siku kama Uviko 19,” amesema.

Naye Mbaraka Shemzigwa ambaye ni Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam tawi la Duce ambaye anasoma kozi ya kudhibiti majanga, amesema anatarajia kuwa kusanyiko hilo la wasomi kutoka Marekani itamsaidia kujua mbinu za kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.

Wakati Dk. Ladislaus Chang’a Mkurugenzi wa Utafiti na Matumizi ya Hali ya Hewa kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), amesema ushirikiano huo utakuwa chachu ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.

“Ushirikiano huu utajibu maswali ya utafiti na namna ya kukabiliana na matatizo ya mabaliko ya tabia ya nchi” amesema Chang’a.

Aidha, Mcole Brasley ambaye ni Mwanafunzi wa Chuo cha Northeastern amesema anatarajia atajifunza mambo mtambuka kuwa kuhusu mabadiliko ya nchi.

Amesema atajifunza sera za uhifadhi wa mazingira na namna bora ya kukabiliana mabadiliko.

1 Comment

  • Tume ya Taifa ya Sayansi ni Tembo Mweupe!
    Tume hii ivunjwe.
    Ziundwe Tume Tano:
    1) Tume ya Utafiti wa Afya iwe sawa na National Institute of Health ya Marekani.
    2) Tume ya Utafiti wa Mazingira iwe sawa na Environmental Protection Agency.
    3) Tume ya Magonjwa ya Milipuko iwe kama Center of Disease Control.
    4) Tume ya Sayansi ishughulike na Sayansi tu.
    5) Tume ya Teknolojia ishughulike na teknolojia tu.
    Bosi wa Uhandisi hawezi kusimamia Afya. Hivyo hiki ni Chuo Kikuu kimoja cha jimbo moja kinakutana na Tume ya Taifa…hakuna hadhi hapa. Vyuo vikutane na vyuo.
    Tume ya Taifa ikutane na Tume ya Taifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Rais Samia kuzindua gazeti litakalotoa habari za wafanyakazi Tanzania

Spread the loveSHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), liko mbioni kufufua...

Habari Mchanganyiko

GGML yaja na teknolojia za kisasa maonesho ya OSHA Arusha

Spread the loveKATIKA kuelimisha wananchi na washiriki wa maonesho ya usalama na...

Habari Mchanganyiko

GGML, OSHA wawanoa mama lishe 50 kukabiliana na majanga ya moto

Spread the loveKampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) kwa kushirikiana na...

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

error: Content is protected !!