Tuesday , 23 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Wadau wajadili changamoto Sheria ya Habari
Habari Mchanganyiko

Wadau wajadili changamoto Sheria ya Habari

Spread the love

WADAU wa habari nchini, wameishauri serikali kuhakikisha sheria zinazokandamiza tasnia ya habari nchini, zinapatiwa ufumbuzi. Anaandika Mwandishi Wetu…(endelea).

Katika mkutano wa mtandaoni uliofanyika leo tarehe 1 Juni 2020, na kuratibiwa na Shirika la Habari la Internews, mtoa mada ya Sheria ya Makosa ya Mtandao (2015), James Marenga ambaye ni Wakili wa Kujitegemea, amesema kuna maeneo kadhaa yanapaswa kufanyiwa kazi ili wanahabari wafanye kazi zao kwa uhuru.

Amesema, Sheria ya Huduma ya Vyombo vya Habari ya sasa, pamoja na kwamba kuna maeneo muhimu na mazuri, lakini kuna vifungu vyenye changamoto kubwa na zenye ukakasi katika utekelezaji wa majukumu ya mwanahabari.

“Vifungu vyenye utata vipo vingi, ni pamoja na kile cha kuweka adhabu kwa makosa ambayo hayako wazi kinyume na Ibara ya 13 (6) (c), kufifisha uhuru wa kupokea na kusambaza habari kinyume na Ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” amesema Marenga.

Katika mkutano huo ulioendeshwa na Anita Mendoza, Kaimu Mtendaji Mkuu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Marenga amesema maeneo mengine yenye ukakasi katika sheria hiyo ni kuathiri uhuru wa faragha kinyume na Ibara ya 16 (1) ya Katiba ya Tanzania.

“Kifungu 3.5 kinaathiri haki ya kusikilizwa kinyume na Ibara ya 13 (6) (a) ya Katiba ya Tanzania. Mfano mwingine kuna kifungu cha 38 (2) (b) cha sheria usikilizwaji wa shauri la mtu bila mtuhumiwa kuwepo. Hivi vifungu na vingine mfano wa hivi, vinatakiwa kufanyiwa marekebisho,” amesema Marenga.

Deodatus Balile, Mkwenyekiti wa TEF na mtoa mada katika kipengele cha Sheria ya Huduma ya Vyombo vya Habari (2016), amesema msisitizo unaendelea kutolewa katika safari ya mabadiko ya sheria za tasnia ya habari nchini.

“Bado uhuru zaidi wa vyombo vya habari unahitajika kama ambavyo mapendekezo yetu ya sheria ya vyombo vya habari yaliyokabidhiwa Dodoma mwaka 2021.

“Msisitizo wetu ni kuona tunafanikiwa malengo. Yapo maeneo mengi ikiwa ni pamoja na kifungu cha 7 (3) (a) kinachompa mamlaka Mkurugenzi wa Habari Maelezo kufuta ama kufungia chombo cha habari,” amesema Balile.

Wadau hao wameeleza, sheria za habari nchini, bado zinaminya uhuru wa vyombo vya habari na kuendelea kutoa mwanya kwa serikali kufungia vyombo vya habari.

Wameeleza, kuna baadhi ya vifungu katika sheria hiyo vinavyowanyima wanahabari haki na uhuru wa kuchapisha taarifa mbalimbali.

Aidha, wanapinga kifungo cha sheria hiyo kinachowataka wanahabari kupewa kibali cha kufanya kazi na kuwepo kwa mamlaka inayoweza kuwazuia wanahabari kupewa kibali hicho.

“Kifungu cha VII kinampa mamlaka mtoa adhabu kutoa adhabu bila ukomo, inapaswa kuwepo na ukomo wa adhabu ya kiwango cha juu na cha chini kama sheria zingine zinavyoelekeza,” amesema Balile.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

NMB yadhamini Mkutano Mkuu ALAT, kufunguliwa na Samia

Spread the loveBENKI ya NMB, imekabidhi hundi yenye thamani ya Sh. 120...

Habari Mchanganyiko

DC ampongeza Dk. Rose Rwakatare kwa kusaidia waathirika wa mafuriko Mlimba

Spread the loveMWENYEKITI wa Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro, Dk.  Rose Rwakatare...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mipango na uwekezaji kutumia bilioni 121.3, mradi wa Bagamoyo wapewa kipaumbele

Spread the loveWIZARA ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, imeliomba Bunge...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mbunge ataka kasi uzalishaji walimu ipunguzwe akidai hakuna ajira

Spread the loveMBUNGE wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi, ameishauri Serikali ipunguze kasi...

error: Content is protected !!