Friday , 17 May 2024
Home Gazeti Habari Haya hapa mapendekezo ya CUF kuhusu katiba, tume huru
HabariHabari za Siasa

Haya hapa mapendekezo ya CUF kuhusu katiba, tume huru

Spread the love

CHAMA cha Wananchi (CUF), kimeshauri mchakato wa katiba mpya uanze mara moja, kikishauri muundo wa Serikali upewe kipaumbele katika kupitiwa upya pamoja na mjadala wa rasimu ya katiba. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Mapendekezo hayo yamewasilishwa leo Jumanne, jijini Dar es Salaam katika Kikosi Kazi kilichoundwa na Rais Samia Suluhu Hassan, kwa ajili ya kukusanya maoni yenye lengo la kuimarisha demokrasia na ujumbe wa CUF, ulioongozwa na Mwenyekiti wake, Prof. Ibrahim Lipumba.

Chama hicho cha upinzani kimeshauri kabla ya mchakato huo kuanza, Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na ya Kura ya Maoni, zifanyiwe marekebisho kwa kuwa zimepitwa na wakati, huku kikipendekeza uundwaji wa tume au kamati maalumu ya watalaamu itakayofanyia kazi rasimu ya tume ya Jaji Joseph Warioba na Katiba Pendekezwa.

“Inawezekana kuunda tume au kamati maalum itakayojumuisha wawakilishi kutoka vyama vya siasa, madhehebu ya dini, Asasi za Kiraia na kupata tume yenye muafaka wa kitaifa. Tume hii itaweka mezani  Rasimu ya Tume ya Jaji Warioba na Katiba inayopendekezwa na kupata Rasimu ya Katiba ya Maridhiano, itakayopitishwa na Bunge na hatimaye kupigiwa kura za Maoni na wananchi,” imesema taarifa ya CUF.

Kuhusu upatikanaji wa tume huru ya uchaguzi, CUF kimependekeza katiba ya sasa ifanyiwe mabadiliko madogo ili kufanikisha upatikanaji wake.

“Kupitia mabadiliko maalum kwenye katiba iliyopo, tume huru ya uchaguzi inayotokana na maoni yaliyokusanywa na tume ya katiba (tume ya Jaji Warioba), iundwe na kuanza kazi mapema. Tume hii isimamie Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na Uchaguzi Mkuu 2025,” imesema taarifa ya CUF.

Katika hatua nyingine, chama hicho kimependekeza masuala mbalimbali kuhusu chaguzi, kikitaka suala la wadhamini kwa wagombea, uhalali wa mawakala wa uchaguzi, yaondolewe kwenye matakwa ya kisheria,  badala yake yaamuliwe na vyama vya siasa.

CUF kimependekeza mapingamizi na rufaa katika chaguzi, yasikilizwe na kutolewa uamuzi ndani ya siku 14, huku kikishauri suala la mgombea kupita bila kupingwa liondolewe badala yake kuwe na kura ya ndiyo au hapana.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Udhibiti wa serikali wakera asasi za kiraia

Spread the loveBaadhi ya wadau wa demokrasia na viongozi wa asasi za...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Nape aomba bajeti ‘kiduchu’ kwa mwaka 2024/25

Spread the loveWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Seneta: Wanasiasa hawasaidii mchakato wa Katiba mpya

Spread the loveSeneta wa jimbo la Busia, nchini Kenya, Okiya Okoiti Andrew...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

ACT-Wazalendo yasusia uchaguzi wa ubunge Zanzibar

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo, kimegoma kushiriki uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo...

error: Content is protected !!