Friday , 17 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Rais Dk.Mwinyi: Mwalimu Nyerere alisisitiza umuhimu wa siasa kujenga uchumi
Habari Mchanganyiko

Rais Dk.Mwinyi: Mwalimu Nyerere alisisitiza umuhimu wa siasa kujenga uchumi

Spread the love

RAIS wa Zanzibar, Dk. Hussein Mwinyi, amesema Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, alisisitiza umuhimu wa siasa katika kujenga uchumi unaojitegemea na matumizi bora ya rasilimali za nchi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Rais Mwinyi ametoa kauli hiyo leo Jumamosi, tarehe 23 Aprili 2022, katika sherehe za kumbukizi ya miaka 100 ya kuzaliwa Mwalimu Nyerere, zilizofanyika nyumbani kwake Msasani, jijini Dar es Salaam.

“Alikuwa ni mwanafalsafa wa masuala mbalimbali ya kiuchumi, kisiasa na kijamii, alitumia uhai wake kusisitiza umuhimu wa kuwa na siasa na mipango ya kujenga uchumi unaojitegemea pamoja na matumizi bora ya rasilimali zetu,” amesema Rais Mwingi.

Rais Mwinyi amesema “aliamini umuhimu wa kuimarisha misingi ya utawala bora kwa kupiga vita vitendo vya rushwa, uzembe, ufisadi na ubadhirifu wa mali za umma.”

Kiongozi huyo wa Tanzania, amesema Mwalimu Nyerere atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa katika ujenzi wa Taifa na ukombozi wa Bara la Afrika.

“Tutamkumbuka kwa namna alivyojitoa mhanga kupigania ukombozi na ujenzi wa Taifa letu, yeye kwa kushirikiana na marehemu Mzee Abeid Karume, ndiyo waliosimamishwa nguzo imara za muungano,” amesema Rais Mwinyi na kuongeza:

“Njia bora zaidi ya kumkumbuka Mwalimu Nyerere ni kutekeleza kwa vitendo urithi aliotuachia pamoja na kumuombea. Kuna mambo mengi ya kujifunza katika kipindi cha miaka 100, kinachojumuisha wakati wa uhai wake na urithi aliotuachia baada ya kifo chake.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Udhibiti wa serikali wakera asasi za kiraia

Spread the loveBaadhi ya wadau wa demokrasia na viongozi wa asasi za...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Nape aomba bajeti ‘kiduchu’ kwa mwaka 2024/25

Spread the loveWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Seneta: Wanasiasa hawasaidii mchakato wa Katiba mpya

Spread the loveSeneta wa jimbo la Busia, nchini Kenya, Okiya Okoiti Andrew...

Habari Mchanganyiko

Wananchi washauriwa kuongeza uelewa wa kujikinga na majanga

Spread the love WITO umetolewa kwa wananchi kuongeza uelewa na utayari kabla...

error: Content is protected !!