Friday , 17 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia achomoa ruzuku vyama vyote vya siasa
Habari za Siasa

Rais Samia achomoa ruzuku vyama vyote vya siasa

Rais Samia Suluhu Hassan
Spread the love

 

RAIS Samia Suluhu Hassan ameonesha kutokukubaliana na mapendekezo ya Kikosi Kazi cha kuratibu maoni ya wadau wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa, kutaka Serikali iangalie uwezekano wa kutoa ruzuku kwa vyama vyote vyenye usajili wa kudumu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Rais Samia amesema kila anayeunda chama anajua atakiendeshaje na kila chama kinakuwa na itikadi yake na kinajua kinaendaje katika kutekeleza majukumu yake.

Rais Samia amesema hayo leo Jumatatu tarehe 21 Machi 2022 baada ya kupokea taarifa ya awali ya kikosi kazi cha kiratibu maoni ya wadau wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa nchini.

“Hivyo vinavyojiendesha vinajiendeshaje? Alihoji Rais Samia na kuongeza, “Unapounda chama cha siasa umejipimaje, utakiendeshaje, unategemea Serikali ikuendeshee chama chako cha siasa? Hapana, ni chama chenu cha siasa mmejiunda sisi itikadi yetu ni hii twendeni tujiendeshe, ruzuku sawa lakini ni kwa wale ambao kweli wanafanyakazi, wapo bungeni wanachapa kazi, unawapa ruzuku ili wajipange wafanye vizuri zaidi lakini hivi vingine je tuviue? Kwahiyo nakuachieni kachemsheni vichwa tuone tunafanya nini na vyama vya siasa na ruzuku.”

1 Comment

  • Kwa hili UMESHINDA!
    Naomba hata kwetu CCM, turudishe viwanja vya michezo kwenye majiji, miji au vijiji.
    Tujiendeshe wenyewe bila unyonyaji au ukupe. Tumiliki majengo tuliyojenga kwa fedha zetu na siyo za serikali.
    Tujiendeshe wenyewe.
    Upo sahihi. Hivi ndivyo vyama vya siasa duniani vnavyojiendesha vyenyewe.
    Pia, nchi zenye demokrasia vyama vinaishia ngazi ya wilaya. Hii inasaidia kuweka serikali za mitaa bila chama au siasa isipokuwa maendeleo ya wananchi na haki ya mazingira mazuri.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Udhibiti wa serikali wakera asasi za kiraia

Spread the loveBaadhi ya wadau wa demokrasia na viongozi wa asasi za...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Nape aomba bajeti ‘kiduchu’ kwa mwaka 2024/25

Spread the loveWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Seneta: Wanasiasa hawasaidii mchakato wa Katiba mpya

Spread the loveSeneta wa jimbo la Busia, nchini Kenya, Okiya Okoiti Andrew...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

ACT-Wazalendo yasusia uchaguzi wa ubunge Zanzibar

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo, kimegoma kushiriki uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo...

error: Content is protected !!