Friday , 17 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Ajali yaua 22 Morogoro, Rais Samia awalilia
Habari MchanganyikoTangulizi

Ajali yaua 22 Morogoro, Rais Samia awalilia

Spread the love

 

WATU 22 wamefariki dunia huku zaidi ya 30 wakijeruhiwa katika ajali ya barabarani ikihusisha basi lenye namba za usajili T 732 ATH mali ya Kampuni ya AHMEED linalofanya safari zake kati ya Mbeya na Tanga kugongana uso kwa uso na lori lenye namba IT 2816 eneo la Melea kibaoni barabara ya Iringa-Morogoro. Anaripoti Mwandishi Wetu, Morogoro … (endelea).

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Fortunatus Muslim amesema, ajali hiyo imetolea Ijumaa ya tarehe 18 Machi 2022 saa 10 jioni wakati basi la Ahmed likitokea Mbeya kwenda Tanga kugongana na lori la lilikokuwa likisafiri kwenda nje ya nchi.

Amesema ajali imetokea wakati lori hilo likijaribu kumkwepa mwendesha pikipiki ndiyo likagongana na basi hilo, yakanasana na kusababisha vifo vya watu 13 papo hapo.

Katika ukurasa wake wa Twitter, Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameandika,”nimesikitishwa na vifo vya watu 22 vilivyosababishwa na ajali ya basi kugongana na lori katika eneo la Melea Kibaoni, Morogoro.”

“Nawapa pole wafiwa, nawaombea marehemu wapumzike mahali pema na majeruhi wapone haraka. Nawasihi watumiaji wa barabara kuzingatia sheria za barabarani.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Udhibiti wa serikali wakera asasi za kiraia

Spread the loveBaadhi ya wadau wa demokrasia na viongozi wa asasi za...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Nape aomba bajeti ‘kiduchu’ kwa mwaka 2024/25

Spread the loveWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Seneta: Wanasiasa hawasaidii mchakato wa Katiba mpya

Spread the loveSeneta wa jimbo la Busia, nchini Kenya, Okiya Okoiti Andrew...

Habari Mchanganyiko

Wananchi washauriwa kuongeza uelewa wa kujikinga na majanga

Spread the love WITO umetolewa kwa wananchi kuongeza uelewa na utayari kabla...

error: Content is protected !!