Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema wadai Spika Tulia anawafanya mazuzu
Habari za SiasaTangulizi

Chadema wadai Spika Tulia anawafanya mazuzu

Dk. Tulia Ackson, Spika wa Bunge la Tanzania
Spread the love

 

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimedai kauli ya Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson, iliyodai Halima Mdee na wenzake 18 wako bungeni kihalali, kwa kuwa hawajawasiisha barua ya kuwafukuza, “ni ulagai wa kisiasa na kutufanya mazuzu”. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo Ijumaa, tarehe 18 Machi 2022 na Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe, akitangaza maazimio ya kikao cha kamati kuu ya chama hicho (CC), iliyoketi hivi karibuni jijini Dar es Salaam.

Mbowe alikuwa akijibu swali na wanahabari kutaka kujua kauli ya chama chake kufuatia hatua ya Spika Tulia kukiri kuwatambua kina Mdee ni wabunge halali wa Chadema.

“Hatuwezi kila siku kuzungumzia wabunge 19, kauli za Spika ni ulaghai wa kisiasa, anajua Spika kwamba wale wabunge hawakutokana na chama chetu na wameshafukuzwa. Ule ni kutufanya sisi mazuzu. Wameshaandikiwa barua na chama kuwa wamefukuzwa,” amesema Mbowe.

Mbowe amesema, kitendo cha wabunge hao 19 kuendelea kubaki Chadema, kinaleta mpasuko kwa Taifa.

“Issue sio kukubali wabunge 19, tunapowakataa wabunge 19 tunakataa ukiukwaji wa sheria za nchi. Forgery (kughushi) iliyofanyiwa Taifa na kwenda kubariki ubatili wa aina hiyo, hatutakubali kutokea,” amesema Mbowe.

Hata hivyo, Mbowe amesema rufaa za wabunge hao zitasikilizwa na kutolewa maamuzi katika kikao cha Baraza Kuu la Chadema, kinachotarajiwa kufanyika tarehe 25 Aprili mwaka huu.

Mbali na Mdee na wengine waliofukuzwa Chadema kwa madai ya usaliti ni, Nusrat Hanje, Grace Tendega. Hawa Mwaifunga, na Jesca Kishoa.

Wengine ni, Agnesta Lambat. Tunza Malapo. Ceciia Pareso, Asia Mwadin Mohamed, Felister Njau, Naghenjwa Kaboyoka, Sophia Mwakagenda, Kunti Majala, Stella Siyao, Salome Makamba, Anatropia Theonest na Conchesta Lwamlaza.

Wabunge hao walivuliwa uanachama wa Chadema tarehe 27 Novemba 2020, siku tatu baada ya kuapishwa na Spika Job Ndugai, kuwa wabunge viti maalumu kupitia chama hicho.

Mdee na wenzake walituhumiwa kwa makosa ya kusaliti msimamo wa Chadema wa kutopeleka wabunge wa viti maalum bungeni, wakipinga matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 28 Oktoba 2020, kwa madai kwamba mchakato wake haukuwa huru na wa haki.

Hata hivyo, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), zilikanusha madai hayo zikisema kwamba ziliendesha mchakato huo katika misingi ya ukweli, haki na uwazi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za SiasaTangulizi

Samia awataka watanzania kudumisha muungano

Spread the loveRais wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan amewataka Watanzania kuendeleza Muungano kwa...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

error: Content is protected !!