Sunday , 19 May 2024
Home Habari Mchanganyiko CCM yaagiza Serikali iangalie upya mwenendo Jeshi la Polisi
Habari Mchanganyiko

CCM yaagiza Serikali iangalie upya mwenendo Jeshi la Polisi

Spread the love

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), imeielekeza Serikali iangalie upya mwenendo wa Jeshi la Polisi, kwa kuwa hauridhishi kutokana na matendo yanayofanywa na baadhi ya maofisa na askari wake kuwa kinyume na muongozo wao wa utendaji kazi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Maelekezo hayo yametolewa leo Jumamosi, tarehe 12 Machi 2022 na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi – CCM, Shaka Hamdu Shaka, akitoa maazimio ya kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya chama hicho, kilichofanyika jana Ijumaa.

“Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM, imeielekeza Serikali kuangalia upya mwenendo wa Jeshi la Polisi nchini, ambao umekuwa hauridhishi na kulalamikiwa na wananchi kutokana na matendo yanayofanywa na baadhi ya maofisa na askari wa jeshi hilo, kinyume na muongozo wa utendaji kazi wa Jeshi la Polisi,” amesema Shaka.

Aidha, Shaka amesema kamati hiyo imempongeza Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kuunda tume ya kuchunguza mauaji ya watu katika Mkoa wa Mtwara na Tanga.

“Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM, imempongeza Rais Samia kwa uamuzi wake wa kuunda tume ya kufuatilia matukio mbalimbali ya uhalifu na kupelekea baadhi ya Watanzania kuuawa katika Mkoa wa Mtwara na Tanga,” amesema Shaka.

1 Comment

  • Hongera sana CCM.
    Polisi wanapokuwa hawapo kazini (off duty) wanajihusisha na ukamataji wa kuwakamua wananchi pesa. Nilitoa mfano wa kona ya Morocco-Mwananyamala.
    Sheria ikataze rasmi kwamba polisi haruhusiwi kusimamisha magari bila sare!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Balile aukwaa uenyekiti wahariri Afrika Mashariki

Spread the loveJumuiya ya Wahariri wa Afrika Mashariki (EAES), imemchagua Mwenyekiti wa...

Habari Mchanganyiko

Jeshi la Uhifadhi kujengewa uwezo zaidi

Spread the love  WIZARA ya Maliasili na Utalii imejipanga vyema kuendelea kulijengea...

Habari Mchanganyiko

Wanavyuo Dodoma waonja utamu wa chimbo la nyuki

Spread the love  TAMASHA la Chimbo la Nyuki lililofanyika katika Ukumbi wa...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Wakili Mwabukusi anusurika kufungiwa, asema hatarudi nyuma

Spread the loveWAKILI Boniface Mwabukusi amesema kuwa hatorudi nyuma kuwatetea Watanzania na...

error: Content is protected !!