Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa CCM kufanya marekebisho ya Katiba yake
Habari za Siasa

CCM kufanya marekebisho ya Katiba yake

Spread the love

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kinatarajia kufanya Mkutano Mkuu Maalumu, kwa ajili ya kufanya marekebisho katiba yake ya 1977, iliyorejewa mwaka 2020, kwa lengo la kujiimarisha kimuundo na kiutendaji ili iendane na wakati. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Taraifa hiyo imetolewa leo Jumamosi, tarehe 12 Machi 2022, jijini Dar es Salaam na Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Shaka Hamdu Shaka, akitoa maazimio ya kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho, kilichofanyika jana Ijumaa.

Amesema mkutano huo unatarajiwa kufanyika tarehe 1 Aprili mwaka huu, kwenye makao makuu ya CCM, jijini Dodoma.

Shaka amesema, tarehe hiyo imependekezwa baada ya kamati hiyo kujadili pendekezo la kuitishwa kwa mkutano mkuu maalumu wa CCM taifa. Mapendekezo hayo yatawasilisha kwa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC).

“Kwa mujibu wa Katiba ya CCM, mamlaka ya kupitisha na kurekebisha katiba yako mikononi kwa mkutano mkuu wa taifa wa CCM, chini ya Ibara ya 99 (5), toleo la 1977, “ amesema Shaka.

Katibu Mwenenzi huyo wa CCM, ametaja malengo matano ya marekebisho hayo, ambayo ni kuongeza ufanisi wa kazi za chama hicho na utekelezaji wa maamuzi ya vikao vyake.

Kupata vioongozi imara, waadilifu na wenye uwezo mkubwa katika kuongoza na kusimamia majukumu ya Serikali za Mitaa, kwa ufanisi.

Mengine ni, kuongeza na kuimarisha udhibiti wa chama kwa viongozi wake wanaochaguliwa kuongoza na kusimamia utekelezwaji wa Ilani ya CCM, kupitia Serikali za Mitaa na kuimarisha nguvu ya chama katika kukabiliana na kudhibiti matumizi mabaya ya madaraka na rushwa.

Lengo la mwisho ni, kuongeza uwakilishi wa jumuiya za CCM ngazi ya kata, kwenye Mkutano Mkuu wa CCM wa Wilaya na kurekebisha itifaki za uwakilishi unaofanana na wenyeviti na makatibu wa jumuiya ngazi yamkoa kuwa wajumbe wa mkutano mkuu wa taifa na wa ngazi ya wilaya kuwa wajumbe wa mkutano mkuu wa mkoa.

Mbali na malengo hayo, Shaka amesema CCM inafanya mabadiliko ya katiba katika kipindi cha kuelekea uchaguzi wake wa ndani, kwa ajili ya kujiimarisha.

“Kwa nyakati hizi ambazo tunaelekea kwenye uchaguzi, niseme ccm tumekuwa na utaratibu wa kujiimarisha nyakato zote tangu 1977 baada ya kuundwa kwake. Kwa vipindi tofauti imekuwa na utaratibu wa kujiimarisha,” amesema shaka.

Shaka amesema “ yako maeneo ambayo kama chama tumehisi bado hatujafanya vizuri, kwa hiyo maeneo hayo tunakwenda kujiimarisha.”

Amesema, marekebisho hayo yatawarejesha Makati wa CCM mikoa kwenye ujumbe wa NEC.

“ Baada ya kufanya tathimini ya kina tulikotoka, tulikopita na muelekeo wetu tunapokwenda, vikao vimeona kwamba kuna haja ya makatibu wa mikoa ambao ni watendaji wakuu wa mikoa kuwa sehemu ya wajumbe wa NEC Taifa, jambo la kuwarudisha makatibu si jambo geni linaendanada na mahitajio ya nyakati tulizo nazo,” amesema Shaka.

Shaka amesema, mkutano huo maalumu utatanguliwa na kikao cha Kamati Kuu ya NEC ya CCM, kitakachofanyika tarehe 31 Machi mwaka huu, jijini Dodoma.

1 Comment

  • Rudisheni miiko ya uongozi la sivyo mtaendelea na ufisadi na rushwa ndani ya CCM
    Ilikuwa kosa kubwa kulitupa Azimio la Arusha pamoja na miiko ya uongozi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

error: Content is protected !!