Saturday , 18 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Vijana wamshinikiza bilionea Dangote kuwania urais
Habari Mchanganyiko

Vijana wamshinikiza bilionea Dangote kuwania urais

Spread the love

 

KUNDI la vijana nchini Nigeria, chini ya mwamvuli wa Bunge la Vijana wa Kaskazini, limetoa wito kwa mfanyabishara tajiri zaidi Afrika, Aliko Dangote, viongozi wengine wa wafanyabiashara na wataalamu kuingilia kati uchaguzi wa rais wa 2023. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Vijana hao wamesema uzoefu wao itasaidia kuleta maendeleo Nigeria.

Katika taarifa kundi hilo ambalo lilifadhiliwa na Katibu Mkuu wake Desmond Minakaro na Baraza la Wawakilishi, Mohammed Salihu Danlami alisema watu kama Dangote, Femi Otedola, Mike Adenuga, Akinwumi Adesina, Herbert Wigwe, Ngozi Okonjo Iweala na kadhalika wana uwezo wa kuchukua nafasi ya rais wa Nigeria.

Wamesema wafanyabiashara wanaojua jinsi ya kupata faida sasa wanapaswa kuitawala Nigeria.

Hata hivyo, Seneta Shehu Sani amesema haoni haja ya Dangote kuingia kwenye siasa na kwamba amemtaka aendelee kuwa maarufu kutokana na utajiri wake.

Kauli ya Seneta huyo imezua gumzo mitandaoni ambapo baadhi ya wachangiaji kama Isha Fola, Joshua Obera, Jibra’eel na @Sirdotskill walisema kwenye akaunti yao ya Twitter kwamba Dangote na vigogo hawa wa biashara huenda wasiweze kuingia katika vituo vyao vya kupigia kura.

Wana mtazamo tofauti wa kisiasa kwa biashara kwa sababu mara nyingi hulinganishwa na kila mmoja.

@jibsunnah aliandika: Biashara na siasa ni vitu viwili tofauti, anaweza akafanikiwa kwenye biashara lakini hatujui anaweza kufanikiwa kwenye siasa, bora ajikite tu kwenye biashara yake.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Balile aukwaa uenyekiti wahariri Afrika Mashariki

Spread the loveJumuiya ya Wahariri wa Afrika Mashariki (EAES), imemchagua Mwenyekiti wa...

Habari Mchanganyiko

Jeshi la Uhifadhi kujengewa uwezo zaidi

Spread the love  WIZARA ya Maliasili na Utalii imejipanga vyema kuendelea kulijengea...

Habari Mchanganyiko

Wanavyuo Dodoma waonja utamu wa chimbo la nyuki

Spread the love  TAMASHA la Chimbo la Nyuki lililofanyika katika Ukumbi wa...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Wakili Mwabukusi anusurika kufungiwa, asema hatarudi nyuma

Spread the loveWAKILI Boniface Mwabukusi amesema kuwa hatorudi nyuma kuwatetea Watanzania na...

error: Content is protected !!