Friday , 26 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Polisi wavunja ukimya utata askari aliyejinyonga mahabusu
Habari MchanganyikoTangulizi

Polisi wavunja ukimya utata askari aliyejinyonga mahabusu

Spread the love

 

JESHI la Polisi limetoa ufafanuzi kuhusu utata wa tukio la kujinyonga hadi kufa kwa Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi, Grayson Mahembe huko mkoani Mtwara, ambapo pamoja na mambo mengine limesema askari anayefariki kwa kujinyonga au kujitoa uhai hazikwi kijeshi. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea)

Kauli hiyo imekuja siku chache baada ya kuibua mjadala kuhusu tukio hilo ambapo Mkaguzi Msaidia huyo aligundulika kujinyonga tarehe 22 Januari, 2022 akiwa mahabusu.

Licha ya Askari huyo kuzikwa tarehe 25 Januari mwaka huu, katika kijiji Iladutwa wilaya ya Iringa mkoani Iringa, maswali mengi yaliibuka kuhusu ndugu kutoshirikishwa, mwili kutopigwa picha, mkanganyiko wa majeraha, mwili kushushwa haraka nyumba kwa mzazi wake Tabata Dar es Salaam na kuzikwa kiraia.

Akizungumzia utata huo leo tarehe 31 Januari, 2022, Msemaji wa Jeshi la Polisi, SACP- David Misime amesema taarifa hizo nyingi ni za kudhania na upotoshaji.

Amesem mijadala hiyo inaonesha watu wamesahau taratibu za mazishi ya askari aliyejinyonga au aliyejitoa uhai wake.

“Askari yeyote anayefariki katika hali ya kujitoa uhai, hazikwi kijeshi, kwa maana kwamba hakuna gwaride la mazishi litakalochezwa na risasi au mabomu ya kishindo kupigwa, kwani anahesabiwa kama hajafa kishujaa na hastahili heshima hiyo.

“Taratibu nyingine hufanyika kama kumpeleka katika eneo atakalozikwa kulingana na matakwa ya familia na ndivyo ilivyofanyika,” amesema.

Aidha, akifafanua kwa kina namna tukio hilo lilivyotokea, Misime amesema Mkaguzi Msaidizi huyo aligundulika kujinyonga tarehe 22 Januari, 2022 akiwa mahabusu kutokana na tuhuma za kukiuka sheria za nchi za kumnyang’anya fedha na kisha kumuua kijana aliyefahamika kwa jina la Mussa Hamis na kisha kuutupa mwili wake vichakani huko katika kijijini cha Namgogori mkoani Mtwara tarehe 5 Januari, 2022.

“Baada ya kufanya tukio hilo la ukiukwaji wa viapo vyao akiwa na wenzake, wakiwepo maafisa, wakaguzi na askari wengine, hawakutoa taarifa kwa viongozi wao kwa sababu walifahamu kuwa wamefanya hivyo kwa nia ovu, kwa tamaa zao na kinyume cha sheria za nchi.

“Baada ya taarifa za tukio hilo kuwafikia viongozi wa Polisi mkoa wa Mtwara, walianza uchunguzi ikiwa ni pamoja na kuwakamata askari waliokuwa wanatuhumiwa,” amesema.

Amesema miongoni mwa askari waliokamatwa na kuanza kuhojiwa ni huyo Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Grayson Mahembe.

Amesema alipohojiwa alielezea mtiririko mzima wa matendo waliyoyafanya na mwisho akawapeleka maafisa waliokuwa wanafanya uchunguzi wa tukio hili sehemu walipoutupa mwili wa Mussa Hamisi na maelezo yake yaliandikwa na yakawa yamelandana na ushahidi mwingine uliokuwa umneshakusanywa.

“Baada ya hatua hiyo aliwekwa katika mahabusu ya peke yake na ndivyo pia ilifanyika kwa wale askari wengine kwani hata baadhi yao ilibidi wapelekwe mahabusu za mkoa wa Lindi ili wasiharibu ushahiri uliokuwa unaendelea kukusanywa.

“Baadaye ndipo ikagundulika kuwa Greyson Mahembe amejingonga. Baada ya tukio hilo taratibu zote za ukaguzi wa matukio zilifuatwa ikiwepo kupiga picha na zipo kwa kututumia wataaalam wa kuchunguza matukio kama hayo.

“Picha hizo zinaonesha dalili zote za mtu aliyejinyonga. Mwili ulifanyiwa uchunguzi pia na daktari wa kuthibitisha kama kifo kilitokana na kujinyonga au sababu zingine.

Ufafanuzi huo wa Polisi umekuja siku chache baada ya baadhi ya wananchi na Baba mzazi wa askari huyo, Gaitan Mahembe kueleza kutoridhishwa na uhalisia wa tukio la mwanaye kujinyonga na taratibu zilizochukuliwa na Jeshi la Polisi.

Akihojiwa na kituo kimoja cha Televisheni, alimuonga Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Simon Sirro kuingilia kati sakata hilo.

Mahembe ambaye ni askari mstaafu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) alihoji mwili wa mwanaye kutopigwa picha kuthibitisha kuwa amejinyonga au lah.

“Polisi walete picha waonyeshe marehemu alikuwa amejinyonga. Ndiyo maana ninamuomba IGP alifafanye. Inasemekana ukweli wake ndiyo uliomponza na ukweli wake ndio uliosababisha hata hao wengine wasemwe,” alisema.

Kuhusu mkanganyiko wa majeraha, Mzee Mahembe alisema ndugu walioneshwa majeraha shingoni mwili ukiwa katika chumba cha maiti.

“Hapo kukawa na korogano ya kwamba si tambara la dekio kama walivyosema. Sasa kwenye mahabusu kuna tambara la dekio, sio mahabusu ya uraiani ni mahabusu ya wao wenyewe polisi.

“Kidogo imenisumbua akili, sijaridhishwa na familia yote haijaridhiswa ninaomba majadiliano, IGP afafanue ukweli, afuatilie ukweli uwe wazi,”alisema.

CHANZO CHA TUKIO

Askari huyo alikuwa miongoni mwa maofisa wa polisi waliokuwa wanashikiliwa kwa tuhuma za mauaji ya mfanyabiashara wa madini, Mussa Hamisi (25) mkazi wa Kijiji cha Ruponda, Nachingwea mkoani Lindi, ambaye anadaiwa kuuawa tarehe 5 mwaka huu.

Inadaiwa kuwa askari hao walimpora mfanyabiasharta huyo madini yenye thamani ya Sh milioni 70 kisha kumuua kwa kumchoma kwa sindano yenye sumu na hatimaye kumtupa katika kitongoji cha Majengo, kijiji cha Hiari wilayani Mtwara.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!