Sunday , 19 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Zitto awaweka sawa viongozi ACT-Wazalendo, awatumia salamu wapinzani
Habari za Siasa

Zitto awaweka sawa viongozi ACT-Wazalendo, awatumia salamu wapinzani

Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo, Ado Shaibu
Spread the love

 

KIONGOZI wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe  amewaagiza viongozi wautumie 2022 kukiimarisha chama  hicho kuanzia ngazi ya Kitaifa hadi mashinani. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Zitto ametoa agizo hilo leo Jumamosi, tarehe 29 Januari 2022, katika Mkutano Mkuu Maalum wa kujaza nafasi ya mwenyekiti wa chama hicho, iliyoachwa wazi na Hayati Maalim Seif Shariff Hamad, uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

“2022 ni wa kujenga chama kama huko uliko una udhaifu wa kiungozi nguo zako nzuri ulizovaa na kofia na atabasamu ulilo nalo halina maana yoyote. Chama ni wanachama kila kiongozi akajitazame huko aliko tukajijenge,”

“chama chetu tukaimarishe kwenye matawi na majimbo. Tukiwa imara kwenye watu hakuna  atakayetuchezea na wala hakutakuwa na wa kukichezea chama chetu,” amesema Zitto.

Licha ya agizo la kukijenga chama hicho, Zitto amewataka viongozi hao wasisahau kuhusu ajenda za kitaifa, ikiwemo madai ya upatikanaji tume huru na katoba mpya.

“Lakini wakati tunajenga chama lazima tuendeleze ajenda za kitaifa, ndiyo ule msemo tunaosema kwetu sisi tunajenga chama wakati tunapambania mabadiliko ya kisheria na kisiasa na tunapigania mabadiliko ya kisheria na kisiasa wakati tunajenga chama sababu hatuna shari ya kuanzia,” amesema Zitto.

Zitto amesema “viongozi wa dini sisi tunatanbua umuhimu wa katiba mpya na tunaipigania katiba mpya, toka  enzi za kina Shaban Mloo, Maalim Seif na Mabele Marando hakuna nyakati ambayo upinzani haujawahi kuipigania na katiba haijapatikana. Lazima twende na yote tunapigania katiba lakini tuhakikishe chaguzi zinazokuja zinasimamiwa na tume huru ya uchaguzi.”

Zitto Kabwe, Kiongozi Mkuu wa ACT-Wazalendo

Aidha, Zitto amesema chama chake kitajiendesha kwa mtindo wa maridhiano kwa kuwa mbinu hiyo itakayowasaidia kupata wanachokitaka.

” Sisi staili yetu ni engagement sababu sisi ni wanasiasa, kwenye siasa lazima ui-engage upate kile unachokitaka. Tutafanya njia zote za ksiasa ku-engage ndiyo maana hatukimbii majadiliano, tunaenda kwenye majadiliano,” amesema Zitto.

Wakati huo huo, Zitto amevitaka vyama vya siasa vya upinzani vikunjue mikono ya maridhiano.

“Licha ya madhila makubwa tuliyopitia katika uchaguzi 2020, tulisema tutaenda kwenye njia ya maridhiano kwa hiyo mtufikishie ujumbe kwa wengine ya kwamba ushirikiano ni two way traffic haiwezekani upande mmoja tu ndiyo kila wakati utoe mkono wa ushirikiano upande mwingine unaweka mkono nyuma,” amesema Zitto na kuongeza:

“Niwashauri muwashauri wengine wakunjue mikono ya mashirikiano, bila mashirikiano hatuwezi kufika kokote. LazIma pande  ziweze kwenda kwa pamoja. Tutaendelea kupambana kuhakikisha tunafanya mabadiliko makubwa katika nchi yetu ili kuhakikisha wananchi wanaishi katika nchi wana furaha nayo.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

CCM yamteua Pele kuwa mgombea ubunge Kwahani

Spread the loveKamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Ujenzi kituo cha kupoza umeme Chalinze wafikia asilimia 93.7

Spread the loveKamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeeleza...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Wakili Mwabukusi anusurika kufungiwa, asema hatarudi nyuma

Spread the loveWAKILI Boniface Mwabukusi amesema kuwa hatorudi nyuma kuwatetea Watanzania na...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

RC Chongolo atangaza ‘vita’ kwa wanaovusha wageni kinyemela

Spread the loveKATIKA kulinda usalama wa nchi kupitia mpaka wa Songwe, Mkuu...

error: Content is protected !!