Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Kodi huduma za mitandaoni yaja
Habari Mchanganyiko

Kodi huduma za mitandaoni yaja

Dk. Mwigulu Nchemba, Waziri wa Fedha na Mipango
Spread the love

 

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba, amesema Serikali itaanzisha ushuru wa huduma za mitandaoni ‘Digital Service Tax’. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Dk. Mwigulu amesema hayo jana tarehe 9 Julai 2021, akihojiwa katika Kituo cha Televisheni cha Azam, jijini Dar es Salaam.

Dk. Mwigulu alisema kodi hiyo itaanzishwa kutokana na kukuaji wa teknolojia, ulioongeza shughuli za biashara mtandaoni.

“Nchi nyingi wanapata fedha nyingi katika eneo hilo, kwa hiyo tunaendelea kulifanyia kazi. Naamini bajeti inayofuata ni eneo ambalo litakuwa ingizo jipya,” alisema Dk. Mwigulu.

Alisema Rais Samia Suluhu Hassan, alipendekeza suala hilo lifanyiwe kazi.

“Hata tulivyokuwa tunafanya briefing (mawasilisho), rais alituelekeza tuangalie eneo hilo sababu mataifa mengi yanageukiwa digital service tax, ambayo inagusa mianya hiyo ya upande wa kukua kwa teknolojia,”

“Hata biashara zipo zinafanyika kwa njia ya kimtandao kwa hiyo ni eneo sahihi, tutakapokuja bajeti zinazofuata tutaliingiza hilo,” alisema Dk. Mwigulu.

Waziri huyo wa fedha alisema, kodi hiyo ilijadiliwa katika bajeti kuu ya Serikali ya mwaka huu wa fedha 2021/22, lakini ilishindikana kuwekwa kutokana na muda kuwa mchache.

“Digital Service Tax ni eneo jipya ambalo tunaendelea kulifanyia kazi, huenda kwenye baadhi ya maeneo tukawa tumechelewa kuyakaweka yote kwenye bajeti hii, lakini ni eneo ambalo tunaendelea kulifanyia kazi,” alisema Dk. Mwigulu na kuongeza:

“itakumbukwa kuwa, tumefanya mabadiliko madogo madogo sababu kile kikapu kizima cha bajeti kimeshapitishwa, kwa hiyo tungehitaji kufumua maeneo mengi sana tungegusa kila mapendekezo tunayopokea.”

Kwa sasa Serikali imeanzisha kodi ya miamala ya simu pamoja na gharama za laini, ambayo imeanza kutumika katika mwaka huu wa fedha kuanzia Julai Mosi 2021.

Kwa mujibu wa kodi hiyo, Serikali itatoza Sh. hadi 200 katika laini za simu, kulingana na matumizi ya salio la mtumiaji.

Pia, itatoza Sh. 10 hadi 10,000 katika kila muamala wa kutuma au kutoa pesa, kulingana na thamani ya muamala wa fedha husika.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

RPC Dodoma akabidhiwa bunduki mbili za wahalifu

Spread the love  Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa ya Kulevya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yazindua huduma maalum kwa wastaafu

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua huduma maalum kwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yazindua akaunti ya Kikundi

Spread the loveBenki ya NMB imezindua akaunti ya kikundi yenye  maboresho makubwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyakazi waidai STAMICO mishahara ya bilioni 1

Spread the loveWALIOKUWA wafanyakazi wa mgodi wa Shirika la Madini la Taifa...

error: Content is protected !!