Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Bajeti 2021/22 kuzipa pumzi NGO’s
Habari Mchanganyiko

Bajeti 2021/22 kuzipa pumzi NGO’s

Spread the love

 

BAJETI Kuu pendekezwa ya Serikali ya Tanzania, kwa mwaka wa fedha wa 2021/22, imekuja na mikakati ya kuzipa nafuu Taasisi Zisizo za Kiserikali (NGO’s), ikiwemo kusamehe kodi ya ongezeko la thamani (VAT), kwenye bidhaa na huduma za miradi inazotekeleza. Anaripoti Nasra Bakari, DMC…(endelea).

Hyao yamesemwa leo Alhamisi, tarehe 10 Juni 2021 na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba, akiwasilisha mapendekezo ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa 2021/22, bungeni jijini Dodoma.

“Napendekeza Kutoa msamaha wa kodi ya ongezeko la thamani, kwa NGO’s, kwenye bidhaa na huduma zitakazotumika kwenye miradi inayotekelezwa na taasisi husika,”

“Aidha, taasisi zitakazonufaika na msamaha huo, ni zile ambazo zina mikataba na Serikali, yenye kipengele kinachotoa msamaha wa kodi ya ongezeko la thamani,” amesema Dk. Mwigulu.

Dk. Mwigulu Nchemba, Waziri wa Fedha na Mipango

Dk. Mwigulu amesema hatua hiyo inalenga kupunguza ukiritimba katika upokeaji wa fedha za misaada za miradi ya maendeleo.

“Kumekwepo na ukiritimba katika kupokea fedha za misaada, kwenye miradi ya maendeleo kwa hitaji la kisheria la kusubiri idhini ya Baraza la Mawaziri likae ili kuidhinisha misamaha,” amesema Dk. Mwigulu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyakazi waidai STAMICO mishahara ya bilioni 1

Spread the loveWALIOKUWA wafanyakazi wa mgodi wa Shirika la Madini la Taifa...

AfyaHabari Mchanganyiko

200 wapimwa afya na GGML katika maonesho ya OSHA

Spread the loveZAIDI ya watu 200 jijini Arusha wamejitokeza kupimwa afya na...

Habari Mchanganyiko

Mfanyakazi CRDB atoa sababu za kubambikiwa kesi, hukumu Mei 30

Spread the love  MFANYAKAZI wa Benki ya CRDB, Ibrahim Masahi (40) ameieleza...

Habari Mchanganyiko

Waziri Ummy atangaza Tanzania kuwa kitovu cha utalii tiba

Spread the loveSERIKALI imesema imedhamiria kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha matibabu ya...

error: Content is protected !!