WAZIRI wa Fedha na Mipango Tanzania, Dk. Mwigulu Nchemba amependekeza kufanya ushuru wa bidhaa ikiwemo bia kuanzia mwaka wa fedha 2021/22. Anaripoti Jemima Samwel, DMC…(endelea).
Akiwasilisha Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2021/22, bungeni jijini Dodoma, leo Alhamisi, tarehe 10 Juni 2021, Dk. Mwigulu amesema “kupunguza ushuru wa bidhaa kwenye bia zinazotengenezwa kwa kutumia shayiri iliyozalishwa hapa nchini kutoka Sh.765 kwa lita za sasa hadi Sh.620 kwa lita.”
amesema “lengo la mapendekezo haya ni kuchochea kilimo cha shayiri hapa nchini.”
Amesema, kuanza kutoza Ushuru wa bidhaa wa asilimia 10 kwenye nyuzi na kamba za plastiki (synthetic fibres) zinazoingizwa kutoka nje ya nchi au kuzalishwa hapa nchini zinazotambuliwa kwa heading 55.11 na 56.07 isipokuwa zile zinazotumika kwenye Uvuvi (HS Code 5607.50.00).
Dk. Mwigulu amesema, lengo la marekebisho haya ni kulinda mazingira na kuchochea uzalishaji na matumizi ya bidhaa za katani. Hatua hii inatarajiwa kuongeza mapato ya Serikali kwa Sh.2,644 milioni.
Waziri huyo amesema, kuanzisha tozo ya ushuru wa bidhaa kwa kiwango cha asilimia 10 kwenye pikipiki zilizotumika kwa zaidi ya miaka 3 zinazoingizwa nchini zinazotambuliwa kwa HS Code 8711.
“Lengo la marekebisho haya ni kudhibiti uingizaji wa pikipiki chakavu na kulinda mazingira. Hatua hii inatarajiwa kuongeza ya mapato ya Serikali kwa Sh.263.7 milioni,” amesema
Leave a comment