Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Lissu atoa masharti matatu kurejea, amjibu IGP Sirro
Habari Mchanganyiko

Lissu atoa masharti matatu kurejea, amjibu IGP Sirro

Tundu Lissu, aliyekuwa Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chadema akiwasili nchini Ubelgiji
Spread the love

TUNDU Lissu, aliyekuwa mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ametoa masharti matatu ili arejee nchini. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Akijibu swali lililomtaka kueleza ni lini atarejea nchini Tanzania, Lissu amesema ni mapema kwa sasa kusema lini atarejea Tanzania na kwamba, kilichomfanya aondoke ni baada ya kutishiwa usalama wa maisha yake.

Ametoa masharti hayo ikiwa ni siku nne kupita baada ya Mkuu wa Jeshi laPolisi nchini, IGP Simon Sirro kumtaka Lissu na Godbless Lemba, aliyekuwa mbunge wa Arusha Mjini kurejea nchini na kwamba, atawalinda.

“Nchi yetu ya amani na utulivu na kama wako nje warudi nchini kuna amani. Ni vizuri Watanzania wakaelewa kwamba, hili ni suala la mtu binafsi  anaamua kusema tu. Kimsingi tukipata taarifa hiyo niko tayari kumpa ulinzi na familia yake, ataishi kwa amani,” alisema IGP Sirro.

Na hata Lissu alipoulizwa, anataka uhakika gani kwa jeshi la polisi ili arejee Tanzania, ametaja mambo matatu kwamba, yakitekelezwa anaweza kurejea nchini.

“…kwanza kesi zote za jinai ziondolewa bila masharti yoyote, pili lazima waseme nani alinipiga risasi na pia waeleze zile kamera za CCTV zilipelekwa wapi?” amesema Lissu leo tarehe 23 Novemba 2020 katika mkutano wake na wanahabari uliofanyika mtandaoni.

Amesema, Desemba mwaka jana chama chake – Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) –  kilimwandikia barua nia yake ya kurejea nchini na kutaka uhakika wa uslama wake, hata hivyo barua hiyo haikujibiwa.

“Desemba mwaka jana tuliandika barua kwa IGP, kumueleza niko tayari kurejea nyumbani, nahitaji usalama kutokana na tishio lakini haijajibiwa, Januari tulikumbusha lakini hatukujibiwa,” amesema Lissu ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Chadema.

Akisisitiza sababu za yeye kurejea, amesema atafanya hivyo iwapo tu jambo la msingi kwake – usalama wake – vitazingatiwa Tanzania hasa baada ya kutishiwa maisha yake baada ya uchaguzi mkuu.

Godbless Lema

“Lini nitarudi…? Nimekuwepo hapa (Ubelgiji) kwa siku hapa 12 tu, sijamaliza hata karantini ya siku 14, ni mapema kusema lini nitarudi. Inategemea na jambo moja muhimu, uhakika wa usalama wangu na maisha yangu.

“…sijakimbia, nimejiokoa maisha yangu, nimejaribiwa kuuawa miaka mitatu iliyopita lakini sasa nitarejea pale tu mazingira yatakuwa salama,” amesema.

Akijibu swali kuhusu kesi zake mahakamani, Lissu amesema kama mahakama iliweza kumsubiri kwa miaka mitatu mpaka akarejea, pia inaweza kumsibiri kwa kipindi kingine kijacho.

“Kesi zitanisubiri, kama walinisubiri kwa miaka mitatu, wanaweza kunisubiri zaidi, kitu muhimu kwangu ni usalama wangu,” amesema.

2 Comments

  • Upo sahihi kabisa Lissu . Wanawezaje kukuhakikishia usalama ukirudi wakati hawajui nani aliyekushambilia mwaka 2017 mchana kweupe!!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yazindua akaunti ya Kikundi

Spread the loveBenki ya NMB imezindua akaunti ya kikundi yenye  maboresho makubwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyakazi waidai STAMICO mishahara ya bilioni 1

Spread the loveWALIOKUWA wafanyakazi wa mgodi wa Shirika la Madini la Taifa...

AfyaHabari Mchanganyiko

200 wapimwa afya na GGML katika maonesho ya OSHA

Spread the loveZAIDI ya watu 200 jijini Arusha wamejitokeza kupimwa afya na...

Habari Mchanganyiko

Mfanyakazi CRDB atoa sababu za kubambikiwa kesi, hukumu Mei 30

Spread the love  MFANYAKAZI wa Benki ya CRDB, Ibrahim Masahi (40) ameieleza...

error: Content is protected !!