December 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Undertaker atandika daluga

Undertaker

Spread the love

BAADA ya miaka 30 ya ubabe na purukushani katika uwanja wa mielekeka, Mark Calaway maarufu kwa jina la Undertaker ameamua kustaafu mchezo huo. Inaripoti BBC … (endelea).

“Kwa miaka 30 nimekuwa nikiingia ndani ya ulingo huu taratibu na kuwaangusha watu mara kwa mara,” Undertaker amesema muda mfupi baada ya kumaliza pambano lake usiku wa Jumapili tarehe 22 Novemba 2020 dhidi ya Survivor Series.

Akihutubia mashabiki wa mieleka wa WWE, Undertaker amesema ‘wakati wa kujiuzulu umefika,” na kuongeza “muda wangu umefika wa kumuacha My time Undertaker apumzike… kwa … amani.”

Katika historia ya WWE, Undertaker anatajwa kuwa mchezaji aliyetumikia mchezo huo kwa miongo mitatu mfululizo kuliko mchezaji mwingine yeyote.

error: Content is protected !!