Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Dk. Tulia akwepa ofisi ya Sugu
Habari za Siasa

Dk. Tulia akwepa ofisi ya Sugu

Spread the love

MBUNGE wa Mbeya Mjini, Dk. Ackson Tulia ameamua kutumia sehemu ya jengo la Mkuu wa Wilaya ya Mbeya kufanya majukumu yake ya kibunge badala ya ofisi ya mbunge. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mbeya…(endelea).

Akieleza sababu za kukwepa ofisi iliyokuwa ikitumiwa na Joseph Mbilinyi maarufu Sugu (Chadema), aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Dk. Tulia amesema ‘nimekwepa mlolongo wa kukabidhiana ofisi.’

“Ningesema nisubiri makabidhiano ya ofisi, nitavuta muda mwingi kama mnavyojua,” amesema Dk. Tulia muda mfupi baada ya kukutana na wananchi na kusikiliza kero zao.

Dk. Tulia Ackson

Dk.  Tulia ambaye ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri, alitangazwa kumshinda Sugu, hata hivyo ushindi wake umeingia ukakasi baada ya Sugu na vyama vya upinzani nchini kukosoa mchakato mzima wa uchaguzi mkuu kwamba, uligubikwa na hila.

Miongoni mwa vipaumbele vya Dk. Tulia kwa wakazi wa jimbo lake ni pamoja na kujenga kiwanda cha taulo za kike, kuimarisha huduma za za afya, kuboresha miundombinu ya elimu, kuboresha soko la wafanyabishara wadogo kwenye eneo la uwanja wa ndege wa zamani.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!