Wednesday , 1 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa JPM: Nataka niwe kama Kikwete
Habari za SiasaTangulizi

JPM: Nataka niwe kama Kikwete

Rais John Magufuli akiwa na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete
Spread the love

DAKTARI John Magufuli, mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), amesema anataka kukaa Ikulu kwa miaka 10 kama Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete ili akamilishe miradi aliyoanzisha. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kishapu … (endelea).

Ametoa kauli hiyo leo tarehe 4 Septemba 2020, wakati akiomba kura wananchi wa Kishapu mkoani Shinyanga, akiwa njiani kuelekea Mara kuendelea na kampeni zake za urais.

Akizungumza na wananchi hao, Dk. Magufuli ameomba apewe tena miaka mitano ili aonyeshe dunia itakavyokwenda.

“Amekuja Mzee Kikwete mmepima kwa miaka 10, mimi miaka mitano ndio maana nawaomba mnipe tena miaka mitano, tuone dunia itakavyokwenda,” amesema Dk. Magufuli.

Amesema, katika kipindi cha miaka mitano ya uongozi wake, ameleta maendeleo licha ya kwamba baadhi ya watu wanabeza utendaji wake.

Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya CCM, John Magufuli akihutubia mkutano wa kampeni Shinyanga

“Tunaingia awamu ya pili ya uchumi, hakuna alietegemea pale Maswa kuwe na viwanda vya chaki, hapa Muwena barabara ya lami nzuri na wanapita watu wa vyama vyote.

“Hata wanaotukana wanapita hapa hapa, shukrani ya punda ni mateke lakini sisi wajibu wetu nikufanya kazi kwa ajili ya Watanzania wote,” amesema Rais Magufuli.

Dk. Magufuli amewaomba wana CCM na Watanzania kwa ujumla kumchagua kwa kuwa, maendeleo hayana chama.

“Ndio maana nawaomba wana CCM wenzangu na wa vyama vingine mtupe kura, sababu maendeleo hayana chama,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

error: Content is protected !!