Wednesday , 22 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Membe awafariji wahanga wa mafuriko
Habari za Siasa

Membe awafariji wahanga wa mafuriko

Spread the love

MGOMBEA Urais wa Tanzania kupitia ACT-Wazalendo, Bernard Membe amewafafiji wahanga wa mafuriko Kata ya Njinjo wilayani Kilwa mkoani Lindi. Anaripoti Faki Sosi, Lindi … (endelea).

Mafuriko hayo yalitokea Januari 2020 na kuathiri kijiji cha Kisimamtika, Kipindimbi na Njinjo na kuharibu makazi na mali za wakazi hao.

Membe akiwa ameambatana na mgombea mwenza Profesa Omar Fakih Hamad wamefika kijijini hapo leo Alhamisi tarehe 3 Septemba 2020 na mwenyeji wao, Shaweji Mketo ambaye ni Mgombea Ubunge Kilwa Kaskazini.

Baada ya kufika eneo hilo, Membe alijionea uharibifu wa makazi ya watu na kuwapa pole.

Ali Ng’ambage mkazi wa Kijiji hicho, amemwambia, Membe tangu kutokea kwa mafuriko hayo kijiji hicho hakina huduma muhimu za kijamii licha ya makazi kuharibika.

Amesema, kijiji hicho hakina huduma za afya, maji safi na salama.

Ng’ambage amesema, serikali haikupata taarifa za ukweli juu ya watu waliofariki kwenye mafuriko hayo.

Mosi Buriani amemwambia Membe kuwa yeye kwenye mafuriko hayo amepoteza mtoto wa Dada yake aliyekuwa akimlea na hadi sasa mwili wake haujapatikana.

“Njinjo tunachangamoto ya madarasa mabovu , Nyumba za walimu hakuna mpaka leo tunalala nje” amesema Mosi huku machozi yakimlenga.

Sina Manolo amesema amefarijika kumuona Membe amewatembelea na kuwapa pole wakazi wa eneo hilo.

Baada ya kuwaona, Membe amesema “Nitakapofika kwenye mkutano nitawaelezeni tutachofanya, nasema poleni kwa yote yaliyowakuta.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Serikali yanawa mikono fidia Kimara-Kibamba

Spread the loveSERIKALI imewataka waathiriwa wa bomoabomoa ya upanuzi wa barabara ya...

Habari za Siasa

Watumishi 25,039, taasisi 65 wahamia Dodoma

Spread the loveSerikali imesema hadi sasa, jumla ya watumishi 25,039 kutoka Serikali...

Habari za SiasaKimataifa

Balozi Kasike ateta na mjumbe wa FRELIMO

Spread the loveBalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Msumbiji, Phaustine...

Habari za Siasa

Watumishi 85,471 walioenguliwa kipindi cha JPM wapandishwa vyeo

Spread the loveSERIKALI imesema kuanzia mwaka wa fedha 2021/2022 hadi sasa jumla...

error: Content is protected !!