Friday , 17 May 2024
Home Kitengo Michezo Mashabiki kuandamana Messi kuondoka Barcelona
Michezo

Mashabiki kuandamana Messi kuondoka Barcelona

Spread the love

BAADA ya mshambuliaji wa klabu ya FC Barcelona, Lionel Messi kutuma maombi maalumu kwa uongozi ya kutaka kuondoka kwenye klabu hiyo, mashabiki wa klabu hiyo wameonekana kujikusanya katika mitaa mbalimbali ya kwenye kitongoji cha Catalunya kuonesha kutokubaliana na jambo hilo. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Jana jumanne 25 Agosti, 2020 mshambuliaji huyo alituma maombi maalumu ya kuondoka kwenye klabu ambayo ameitumikia kwenye maisha yake yote kwenye mchezo wake wa soka.

Taarifa kutoka katika vyanzo mbalimbali zinaeleza kuwa bodi ya klabu hiyo huwenda ikakutana hivi karibuni na pengine Rais wa klabu hiyo Josep Maria Bartomeu’s akajiuzuru kutokana na kuonekana ndiyo sababu kubwa ya mchezaji huyo kuchukua maamuzi hayo.

Kilichopo kwa sasa kati ya Messi na jopo lake pamoja na klabu ya Barcelona ni kuwekana sawa katika vipengele cha mkataba, ambapo moja ya kipengele kwenye mkataba wake ni endapo kama kuna klabu yoyote itamtaka huduma ya mchezaji huyo itoe kiasi cha Tsh. 1.9 trilioni.

Lionel Messi

Messi amechukua maamuzi hayo baada ya kupoteza kwenye mchezo wa nusu fainali ya Klabu Bingwa Ulaya kwa mabao 8-2 dhidi ya klabu ya FC Bayern kutoka Ujerumani na uongozi kuamua kumtimua kocha wao Quique Setien.

Tayari klabu hiyo imeshamtangaza, Ronald Koeman kuja kuchukua mikoba ya Setien licha ya Messi kukataa kufanya mazungmzo naye na kumueleza kuwa anataka kuhama kwenye klabu hiyo.

Lakini pia ameonekana kutokuwa na furaha kutokana na jinsi kocha huyo mpya alivyosema kuwa hana mpango wa kumtumia Luis Suarez ambaye ni swahiba mkubwa wa Lionel Messi.

Mashabiki wengi wa klabu hiyo wameonekana kutokukubaliana na swala hilo na kumtaka Rais wa klabu hiyo Bartomeus kuachia ngazi mara moja ili kumnusuru mshambuliaji huyo kuondoka kwenye klabu hiyo.

Messi mwenye umri wa miaka 33 alijiunga katika shule ya kukuza vipaji ya Barcelona toka 2001, na kuitumikia klabu hiyo kwa mafanikio makubwa huku akishinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia ‘Ballon D’or’ mara sita akiwa mbele ya Cristiano Ronaldo alitwaa tuzo hiyo mara tano.

Aidha Messi amefanikiwa kutwaa taji la Ligi Kuu nchini Hispania mara 10, klabu bingwa Ulaya mara nne, kombe la Ligi mara sita, klabu bingwa dunia mara tatu na tuzo ya mchezaji bora wa Ligi kuu nchini mara nane.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Uingereza, Hispania, Italia na Ufaransa kinawaka leo

Spread the loveLIGI mbalimbali barani ulaya kuendelea leo na michezokadhaa mikali itakwenda...

Michezo

Leo mkwanja upo Meridianbet, usipishane nao

Spread the love  Siku ya leo ni nzuri sana kwa wewe mtumiaji...

Michezo

Anza wikendi yako na Meridianbet, upige mkwanja wa maana

Spread the love Siku ya leo ni nzuri sana kwa wewe mtumiaji...

Habari MchanganyikoMichezo

Arafat atoka bima na kurejea kwenye benki

Spread the loveRais wa Zanzibar Hussein Mwinyi amemteua Arafat Ally Haji kuwa...

error: Content is protected !!