Saturday , 4 May 2024
Home Habari Mchanganyiko DIT inavyojipanga kukabili soko la ajira
Habari Mchanganyiko

DIT inavyojipanga kukabili soko la ajira

Spread the love

TAASISI ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) inakusudia kuboresha mitaala ya shahada mbili za umahiri (masters) ili kuendana na ushindani wa soko la ajira ndani na nje. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Pia, lengo la maboresho hayo ni kuwawezesha wahitimu kuwa na uwezo mkubwa ikiwemo kujiajiri.

Jana Jumanne tarehe 11 Agosti 2020, DIT ilikutana na wadau mbalimbali ili kujadiliana jinsi ya kuboresha mitaala hiyo.

Shahada zinazoboreshwa ni Master of Computational Science and Engineering-MCSE na Master of Maintenance in Engineering and Management-MENG).

Mkuu wa Idara ya Masomo ya Umahiri, Utafiti na Machapisho wa DIT, Profesa Leonia Henry, anasema kuwa wataangalia eneo la ufundishaji, vifaa vinavyotumika kufundishia na maendeleo ya kidijitali.

“Mchakato huu ukikamilika, mitaala iliyoboreshwa itaanza kutumika katika mwaka mpya wa masomo unaonza Novemba 2020,” alisema Profesa Leonia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

RPC Dodoma akabidhiwa bunduki mbili za wahalifu

Spread the love  Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa ya Kulevya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yazindua huduma maalum kwa wastaafu

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua huduma maalum kwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yazindua akaunti ya Kikundi

Spread the loveBenki ya NMB imezindua akaunti ya kikundi yenye  maboresho makubwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyakazi waidai STAMICO mishahara ya bilioni 1

Spread the loveWALIOKUWA wafanyakazi wa mgodi wa Shirika la Madini la Taifa...

error: Content is protected !!