Saturday , 20 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Biden ateua mgombea mwenza mweusi
Kimataifa

Biden ateua mgombea mwenza mweusi

Kamala Harris
Spread the love

JOE Biden, mgombea urais kupitia Chama cha Democratic nchini Marekani, amemteua Kamala Harris, Seneta wa California kuwa mgombea mwenza wake. Inaripoti mitandao ya kimataifa … (endelea).

Kamala anakuwa mwanamke wa kwanza mweusi nchini Marekani kuteuliwa kuwa mgombea mwenza wa urais.

Uchaguzi Mkuu nchini humo unatarajiwa kufanyika tarehe 3 Novemba 2020.

Kamala ambaye aliwahi kuwa mwanasheria mkuu wa Califonia, ana asili ya India na Jamaica.

Pia, aliwahi kumwendesha puta Biden wakati wa kusaka mgombea urais ndani ya chama hicho.

Biden ameelezwa kumpendekeza na kumteua Kamala kutokana na msimamo wake hasa wa kutaka mageuzi ndani ya Jeshi la Polisi nchini humo dhidi ya ubaguzi wa rangi.

Joe Biden

Pia ni miongoni mwa viongozi wa juu nchini humo walioshiriki kutuhumu ubaguzi wa rangi wakati wa kampeni ya Black Live Matter.

Kalama anatarajiwa kukutana jukwa moja na mgombea mwenza wa Donald Trump wa Chama cha Republican – Mike Pence tarehe 7 Oktoba 2020 katika mji wa Salt Lake, Utah.

Historia inaonesha, wanawake wawili waliowahi kuteuliwa kuwa wagombea wenza wa kiti cha urais Marekani, Sarah Palin wa Republican (2008) na Geraldine Ferraro wa Democrats (1984), wote wazungu lakini hawakuwahi kufanikiwa kuingia Ikulu ya Marekani.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!