Wednesday , 22 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Magufuli achukua fomu kuwania urais Tanzania
Habari za SiasaTangulizi

Magufuli achukua fomu kuwania urais Tanzania

Spread the love

DAKTARI John Pombe Magufuli amechukua fomu ya kuwania urais wa nchi hiyo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo Alhamisi tarehe 6 Agosti 2020 katika Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) zilizopo Ndejengwa jijini Dodoma. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Magufuli ambaye ni Rais wa Tanzania, ameambatana na mgombea mwenza, Samia Suluhu Hassa na viongozi mbalimbali wa CCM akiwemo Dk. Bashiru Ally, katibu mkuu wa chama hicho na Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa.

Magufuli amekabidhi fomu hizo na Jaji Semistocles Kaijage, Mwenyekiti wa NEC kwa gharama ya Sh.1 milioni.

Magufuli amekuwa mgombea wan ne wa nafasi hiyo kuchukua fomu akitanguliwa na, Seif Maalim Seif wa Chama cha Alliance for African Farmers Party (AAFP), Philipo John Fumbo wa Chama cha Democratic Party (DP) na Leopold Mahona wa Chama cha National Reconstruction Alliance (NRA).

 

Shughuli ya uchukuaji na urejeshaji wa fomu, umeanza jana Jumatano hadi tarehe 25 Agosti 2020 siku ambayo utafanyika uteuzi.

Tarehe 26 Agosti hadi 27 Oktoba 2020 kitakuwa kipindi cha kampeni na Jumatano 28 Oktoba 2020 itakuwa ni siku ya upigaji kura.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaKimataifaTangulizi

Waliowekewa damu yenye VVU, homa ya ini kulipwa fidia trilioni 32.9

Spread the loveWaziri mkuu wa Uingereza, Rishi Sunak ameahidi kulipa fidia ya...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali yanawa mikono fidia Kimara-Kibamba

Spread the loveSERIKALI imewataka waathiriwa wa bomoabomoa ya upanuzi wa barabara ya...

Habari za Siasa

Watumishi 25,039, taasisi 65 wahamia Dodoma

Spread the loveSerikali imesema hadi sasa, jumla ya watumishi 25,039 kutoka Serikali...

Habari za SiasaKimataifa

Balozi Kasike ateta na mjumbe wa FRELIMO

Spread the loveBalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Msumbiji, Phaustine...

error: Content is protected !!