Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Marekani ‘yapora’ Jumba la Yahya Jammeh
Habari za Siasa

Marekani ‘yapora’ Jumba la Yahya Jammeh

Spread the love

JUMBA la kifahari la Yahya Jammeh, aliyekuwa Rais wa Gambia, limechukuliwa na Serikali ya Marekani. Inaripoti mitandao ya kimataifa…(endelea).

Kwa mujibu wa taarifa za Wizara ya Sheria Marekani, Jammeh alikwapua fedha za umma wakati akiwa madarakani na kununua jumba hilo la kifahari lililopo Washington DC.

Wizara hiyo inaeleza, Jammeha alifanya ufisadi ndani ya Serikali yake na kununua jumba hilo lenye dhamani ya Dola za Marekani milioni 3.5miaka 10 iliyopita.

Uchanguuzi wa wizara hiyo umeeleza kubaini kwamba, Jammeh alinunua jumba hilo kupitia jina la mke wake Zineb Jammeh.

Mwanasiasa huyo mtata, alitoroka Gambia baada ya kushindwa kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2017, kwa sasa anaishi nchini Equatorial Guinea.

Jammeh aliyezaliwa Mei 1965, aliingia madarakani baada ya mapinduzi mwaka 1994. Mwaka 2007 alitangaza kwamba, anaweza kutibu UKIMWI na ugumba kwa kutumia dawa za mitishamba.

Mwaka 2008, alitangaza kuwa atanyonga wapenzi wa jinsia moja na mwaka 2013, aliapa kuendelea kuongoza taifa hilo miaka bilioni kama ataendelea kuwa hai.

Awali, Jammeh aligoma kuondoka madarakani madarakani baada ya kushindwa kwenye uchaguzi 2017 na mpinzani wake Adama Barrow.

Kisha alitangaza hali ya tahadhari kwa siku 90, akisema Tume ya Uchaguzi nchini humo ilitenda makossa katika kuendesha na kuhesabu kura.

Wakati huo, hofu ya kisiasa ilikuwa imetanda nchini humo kiasi cha raia wake wengi kutorokea nchi jirani wakihofia kuzuka kwa maigano.

Mataifa ya Afrika Magharibi yaliwatuma wanajeshi Gambia na kutishia kumuondoa Jammeh madarakani kwa nguvu.

Hata hivyo, Jammeh aliyeiongoza Gambia kwa miaka 22, alikubali kung’atuka na kuondoka nchini humo baada ya Rais Adama Barrow ameapishwa.

Siku moja baada ya kuachia madaraka kwa Adama Barrow, Yahya Jammeh alihamia Equatorial Guinea.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Sabaya afutiwa kesi, ruksa kugombea uongozi

Spread the loveMwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP leo Ijumaa amefuta rufaa...

Habari za Siasa

Serikali yasaka bilioni 3 kujenga daraja Mto Mpiji

Spread the loveSerikali imesema inaendelea na juhudi za kutafuta fedha kiasi cha...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kwafukuta kisa chaguzi, Lissu aibua tuhuma nzito

Spread the loveCHAGUZI za kusaka viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

error: Content is protected !!