Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Wabunge wengine kuondoka Chadema
Habari za SiasaTangulizi

Wabunge wengine kuondoka Chadema

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema
Spread the love

TAKRIBANI wabunge wengine watano kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wako mbioni kukihama chama hicho. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa zinasema, wabunge wote watano, wanaweza kutangaza kuondoka Chadema, muda wowote kutoka sasa.

Kwa mujibu wa gazeti la kila wiki la RAIA MWEMA, kuondoka kwa wabunge hao kunatokana na sababu mbalimbali, ikiwamo madai ya “kutengwa” na baadhi ya viongozi wao wakuu wa chama.”

Madai mengine yanayotajwa kuwa sababisho la kuondoka kwao, ni kutoheshimiwa kwa mchango wao ndani ya chama, makundi yanayotokana na uteuzi wa wabunge ya viti maalum na ubaguzi.

Miongoni mwa wanaotajwa kutaka kuondoka, wapo wabunge watatu wa majimbo na wawili wa viti maalum.

Wabunge wawili wa viti maalum, mmoja anatarajiwa kujiunga na chama cha NCCR- Mageuzi na mwingine anaweza kuelekea ACT- Wazalendo.

“Wale wa majimbo, wanakwenda Chama Cha Mapinduzi (CCM),” kimeeleza chanzo cha taarifa.

Kila mmoja amekuwa akifanya majadiliano na viongozi wa vyama wanavyotaka kujiunga navyo.

Ikiwa wabunge hao wataondoka, basi chama hicho, kitakuwa kimepoteza wabunge 25 tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani wa 25 Oktoba 2015.

Mpaka sasa, Chadema kimeshapoteza wabunge 20 kati ya 71 waliopatikana katika uchaguzi huo.

Katika orodha ya waliokwishaondoka, wapo waliojiuzulu wenyewe kwa kile walichoita, “kuunga mkono juhudi,” wapo waliofukuzwa kwenye chama; wapo waliovuliwa ubunge na mahakama na yupo aliyefariki dunia.

Wabunge waliounga mkono juhudi, ni mbunge wa Ukonga, Mwita Mwaikabe Waitara; mbunge wa Siha, Dk. Godwin Mollel; mbunge wa Babati Mjini, Pauline Gekul na nbunge wa Monduli, Julius Kalanga.

 

 

Wengine, ni mbunge wa Serengeti, Ryoba Marwa; mbunge wa Ukerewe, Joseph Mkundi na mbunge wa Simanjiro, James Ole Millya.

Aliyekuwa mbunge wa Moshi Vijijini, Anthony Komu na aliyekuwa mbunge wa Rombo, Joseph Selasini, walitangaza kuondoka Chadema na kujiunga na NCCR- Mageuzi, mara baada ya kumaliza kipindi chao cha ubunge.

Hata hivyo, baadaye Chadema kilitangaza kuwafuta uwanachama. Mwingine aliyefukuzwa uwanachama, ni Willfred Lwakatare.

Mbunge wa Buyungu mkoani Kigoma, Mwalimu Kasuku Bilago, alifariki dunia. Bilago alikutwa na mauti, mchana wa tarehe 26 Mei 2018, akiwa katika hospitali ya taifa Muhimbili, alikokuwa akipatiwa matibabu.

Aliyekuwa mbunge wa Ndanda, Cecil Mwambe, aliondoka chama hicho tarehe 15 Februari 2020 na kujiunga na CCM.

Aliyekuwa mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na mwenzake wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari, waliong’olewa bungeni na Spika wa Bunge, Job Ndugai kwa madai ya “utoro bungeni.”

Katika orodha hiyo, wapo waliondoka katika siku za mwisho za kumalizika kwa mkutano wa 19 wa Bunge. Waliondoka bungeni, ni Peter Lijualikali, David Silinde, Anna Gidarya, Dk. Sware Semesi na Latifa Chande.

Miongoni mwa wanaotajwa kuondoka sasa, ni pamoja na mbunge wa Karatu, mkoani Arusha, Willy Qulwi Qambalo.

Katika siku za hivi karibuni, Qambalo amekuwa na mvutano mkubwa na chama chake, unaotokana na hatua yake ya kuingia bungeni wakati chama hicho, kimezuia wabunge wake, kuhudhuria mkutano wa bunge la bajeti kwa maelezo ya kujikinga na Corona.

Aidha, Qambalo alikuwa mmoja wa wabunge wa Chadema waliopigia kura ya NDIO bajeti kuu ya serikali.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Sabaya afutiwa kesi, ruksa kugombea uongozi

Spread the loveMwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP leo Ijumaa amefuta rufaa...

Habari za Siasa

Serikali yasaka bilioni 3 kujenga daraja Mto Mpiji

Spread the loveSerikali imesema inaendelea na juhudi za kutafuta fedha kiasi cha...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kwafukuta kisa chaguzi, Lissu aibua tuhuma nzito

Spread the loveCHAGUZI za kusaka viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo...

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga “HIDAYA” chaendelea kuimarika, wananchi wapewa tahadhari

Spread the loveMAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kutoa taarifa...

error: Content is protected !!