Sunday , 28 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Mchimbaji Tanzanite aibuka bilionea, JPM ataka alipwe
Habari Mchanganyiko

Mchimbaji Tanzanite aibuka bilionea, JPM ataka alipwe

Spread the love

SANINIU Laizer, amekuwa Mtanzania wa kwanza kuvunja rekodi ya uchimbaji mawe makubwa ya madini ya Tanzanite, yenye thamani ya Sh. 7.8 bilioni. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Leo Jumatano tarehe 24 Juni 2020, Laizer ameyakabidhi mawe hayo kwa Dotto Biteko, Waziri wa Madini na Dk. Ashatu Kijaji, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, katika Migodi  ya Tanzanite Mirerani, wilayani Simanjiro mkoa wa Manyara.

Jiwe la kwanza lina kilo 9.2 ambalo lina thamani ya Sh. 4.5 bilioni na la pili lenye kilo 5.8 lina thamani ya Sh. 3.3 bilioni.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa mawe hayo, Waziri Biteko amesema, Rais John Magufuli ameagiza madini hayo yanunuliwe na Serikali, kisha yakahifadhiwe katika makumbusho kwa ajili ya kuweka historia.

“Rais Magufuli alinipigia simu akanipa maelekezo, akasema hayo mawe msipoyanunua nyie serikali, yatanunuliwa na wageni.”

“Akasema hapana, hatuna shida ya fedha na mchimbaji asidhurumiwe hata shilingi moja yake, ndio maana tumekuja wote, Gavana wa Benki Kuu (BoT) yupo hapa, wizara ya fedha iko hapa,” amesema Waziri Biteko

“Tusipoyanunua yatatoka Tanzania lakini tutafunga safari kwenda kuyaangalia mawe makubwa nje. Ili kuonyesha kwamba Tanzania tuna madini, Rais kasema yanunuliwe, tutaweka katika makumbusho yetu ili watu waangalie kweli Tanzania ni kiini cha Tanzanite dunian,” amesema

Rais Magufuli akizungumza na umati wa watu waliojitokeza katika shughuli hiyo kwa kutumia simu ya Waziri Biteko amesema, “kwanza nampongeza sana huyo Laizer nah ii ndiyo faida ya wachimbaji wadogo wadogo.”

“Na hii ni kudhihirisha kwamba sisi ni matajiri, nampongeza wewe waziri wa madini (Biteko), wizara ya fedha, gavana na wananchi wa Simanjiro,” amesema Rais Magufuli huku akishangiliwa na wananchi waliokuwapo

Rais Magufuli alimtania Laizer kuwa anajua anakwenda kutafuta mwanamke mwingine, akatafute hata mwanamke wa Kisukuma.

Kwa upande wake, Dk. Kijaji amesema Laizer atakabidhiwa fedha hizo leo.

“Bil. 8 ni kitu gani kwa Rais Magufuli? tunazo hapa ndio maana tunae mlipaji wa serikali, Laizer leo hatumpi karatasi anakabidhiwa fedha zake,” amesema Dk. Kijaji.

2 Comments

  • Daaah haki iko wapi ??
    Fanyeni haki police msitumie madaraka tofauti na itikadi za sheria.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NBC yapata tuzo ya mwezeshaji bora wa mikopo serikali Afrika

Spread the loveBenki ya NBC imepata tuzo ya Mwezeshaji Bora wa Pamoja...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Biteko aipongeza GGML kudhibiti vifo, majeruhi mahali pa kazi

Spread the loveNAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari Mchanganyiko

Wami Ruvu hawana deni la Rais Samia katika kutunza vyanzo vya maji

Spread the love  BODI ya Maji Bonde la Wami Ruvu, imeendelea kuchua...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

error: Content is protected !!