Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Maisha Afya Watanzania watahadharishwa na Corona
Afya

Watanzania watahadharishwa na Corona

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu
Spread the love

SERIKALI ya Tanzania imetahadharisha wananchi wake, juu ya hatari ya ugonjwa wa Covid-19 unaosababishwa na mlipuko wa Virusi  vya Corona, unaotikisa dunia hivi sasa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumza na wanahabari leo tarehe 29 Februari 2020, Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya, amewataka Watanzania kuepuka vitendo vinavyoweza pelekea maambukizi ya ugonjwa huo.

Waziri Ummy amewataka Watanzania, kukwepa, kupeana mikono,  kukumbatiana na kupigana mabusu, katika kipindi hiki ambacho mlipuko huo umeshika kasi.

“Katika kipindi hiki ambacho kuna tishio la ugonjwa wa Corona, ninawataka wananchi kujizuia kupeana mikono, kukumbatiana na kubusiana hili linaweza kuwa gumu kwa Watanzania ila lazima niliseme,” amesema Waziri Ummy.

Wakati huo huo, Waziri Ummy  ametoa siku tatu kwa kila Mkoa nchini, kuwasilisha jina la kituo maalumu,  kilichotengwa kwa ajili ya kuhudumia washukiwa au wagonjwa wa Covid-19.

Hadi sasa virusi hivyo vimesambaa zaidi ya nchi 50 duniani, na kuuwa maelfu ya watu. Huku nchi ya China ikiwa mhanga mkubwa wa ugonjwa huo.

Hata hivyo, Waziri Ummy amesema Tanzania haina mgonjwa wa Covid-19.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari Mchanganyiko

200 wapimwa afya na GGML katika maonesho ya OSHA

Spread the loveZAIDI ya watu 200 jijini Arusha wamejitokeza kupimwa afya na...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

AfyaHabari Mchanganyiko

Songwe katika mikakati ya elimu ya lishe kudhibiti udumavu

Spread the love  SERIKALI mkoani Songwe imejipanga kuendelea kutoa elimu ya lishe...

Afya

Mloganzila yajipanga kupandikizaji wa ini

Spread the love  HOSPITALI ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imesema kutokana na uwekezaji uliofanywa...

error: Content is protected !!