Sunday , 28 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Waganga wa jadi watapeliwa Mil 5
Habari Mchanganyiko

Waganga wa jadi watapeliwa Mil 5

Sehemu ya vifaa vya waganga wapiga ramli
Spread the love

WAGANGA 40 wa tiba asili na tiba mbadala, wametapeliwa kiasi cha Sh. 5.2 Mil na watu waliojifanya kuwa viongozi wa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala (UWAWATA). Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma…(endelea).

Utapeli huo umeelezwa leo tarehe 14 Januari 2020 na Lukas Mlipu, Katibu Mkuu wa UWAWATA Taifa kwenye semina ya siku mbili ya waganga wa tiba asili na tiba mbadala Kondoa, Dodoma.

Semina hiyo ililenga kuwahamasisha kujitambua na kuwatambua waganga, matapeli pamoja na kufanya kazi kwa kuwa na vibali vinavyotambulika.

Mlipu amesema, waganga 40 wa Wilaya ya Kondoa walikuwa wakifanya shughuli zao bila vinali vya usajili, na badala yake walikuwa wakitumia vinali feki walivyovipata kupitia wa matapeli waliojifanya viongozi wa UWAWATA.

Katika semina hiyo, baadhi ya waganga wa tiba asili na tiba mbadala walisema, walilazimika kukata vibali vya utambulisho kwa Sh 130,000 kutoka kwa watu waliokuwa wakijinasibu kuwa ni viongozi wa UWAWATA.

Alisema, kwa sasa wameibuka mapapeli na kujihusisha na kazi za kutoa huduma ya tiba asili na tiba mbadala, pia kufanya vitu vya ajabu, jambo ambalo linalochangia kuharibu tasinia hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wami Ruvu hawana deni la Rais Samia katika kutunza vyanzo vya maji

Spread the love  BODI ya Maji Bonde la Wami Ruvu, imeendelea kuchua...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

Habari Mchanganyiko

Dk. Jafo aipongeza Oryx kumuunga mkono Samia

Spread the loveWAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na...

Habari Mchanganyiko

Mvungi aendesha kikao kazi cha wataalam wa Regrow

Spread the love  MKURUGENZI wa Idara Sera na Mipango Wizara ya Maliasili...

error: Content is protected !!