Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Jibu la hekima la Prof. Assad
Habari za SiasaTangulizi

Jibu la hekima la Prof. Assad

Aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Assad Mussa (kulia) akimkaribisha CAG mpya, Charles Kichere ofisi muda mchache kabla ya kumkabidhi ofisi hiyo
Spread the love

PROFESA Mussa Assad, aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG), anatarajiwa kukabidhi ofisi leo tarehe 5 Novemba 2019. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Hata hivyo, amesema ‘sina kinyongo’ baada ya kuhojiwa na vyombo mbalimbali vya habari kuhusu ‘kustaafishwa’ kwake kwa mujibu wa Ikulu, jijini Dar es Salaam.

“Kwa kuwa nimefanya kazi kwa uadilifu, nadhani kusamehe ni bora zaidi, sina kinyongo. Sijawahi kabisha kumtengenezea mtu maudhi, sasa najiandaa kufuga kuku,” amesema Prof. Assad alizungumza tarehe 4 Novemba 2019 .

Mtaalamu huyo mbobezi katika masuala ya ukaguzi, alitenguliwa kwenye nafasi hiyo na Rais John Magufuli tarehe 3 Novemba 2019, kabla ya kupewa barua ya utenguzi huo.

Taarifa ya kutenguliwa kwake ilitangazwa na Balozi John Kijazi, Katibu Mkuu Kiongozi ambapo ilieleza, Charles Kichere kuchukua nafasi hiyo.

Leo tarehe 5 Novemba 2019, Prof. Assad amekutana na Kichere na kukabidhi taasisi na kwamba, makabidhiano rasmi yatafanyika Dodoma.

“Mimi nimepokea ofisi hii kutoka kwa bwana Uttoh (Ludovick Uttoh) five years ago (miaka mitano iliyopita), naamini sikufanya energy destructions (uharibifu).

“Mimi huwa naamini changes (mabadiliko) zinaweza kutokea, lakini zitokee kwa namna zilivyopangwa vizuri, si mwaminifu wa kutoa watu wote and then (halafu) unaweka new team (watu wapya),” amesema Prof. Assad wakati wa makabidhiano hayo ya awali.

Awali, akizungumza namna alivyoshirikiana na watumishi wengine Prof. Assad alisema, hana kumbukumbu ya kumtendea uovu mtu yeyote kwa kudhamiria katika maisha yake, na kwamba huwenda kuna watu walioteseka kwa kutenda uadilifu.

Alieleza kuwahi kuwaachisha kazi wafanyakazi wanne kutokana na wizi, na kwamba ilikuwa hitajio la kisheria kwa kuwa waliofukuzwa walikutwa na hatia.

Prof. Assad aliyeingia kwenye nafasi hiyo baada ya kuteuliwa na Rais Jakaya Kikwete tarehe 1 Desemba 2014 amesema, hatofanya kazi yoyote serikali kwa kuwa, Katiba ya Jamhuri inazuia CAG kufanya kazi yoyote serikalini baada ya kuondoka mamlakani.

Akifafanua zaidi, CAG amesema anajiandaa kwenda kufuga kuku sambamba na kuendeleza kilimo. Amesema, “sasa nakwenda kufuga kuku na kulima, tuna mashamba makubwa.”

Prof. Assad (58) aliondolewa madarakani tarehe 3 Novemba 2019, akiwa kwenye mkutano wa sita wa Taasisi za Fedha za Kiislamu barani Afrika.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Sabaya afutiwa kesi, ruksa kugombea uongozi

Spread the loveMwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP leo Ijumaa amefuta rufaa...

Habari za Siasa

Serikali yasaka bilioni 3 kujenga daraja Mto Mpiji

Spread the loveSerikali imesema inaendelea na juhudi za kutafuta fedha kiasi cha...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kwafukuta kisa chaguzi, Lissu aibua tuhuma nzito

Spread the loveCHAGUZI za kusaka viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo...

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga “HIDAYA” chaendelea kuimarika, wananchi wapewa tahadhari

Spread the loveMAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kutoa taarifa...

error: Content is protected !!