Saturday , 4 May 2024
Home Kitengo Maisha Afya Waziri Ummy aijia juu MSD
AfyaTangulizi

Waziri Ummy aijia juu MSD

Spread the love

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeitaka Bohari Kuu ya Dawa nchini (MSD) kuhakikisha wanakamilisha kuleta vifaa vyote vinavyohitajika katika vituo vya Afya vinavyoboreshwa nchini kabla ya Januari 15, 2019 ili wananchi waweze kupata huduma. Anaripoti Mwandishi Wetu, Misungwi … (endelea).

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy wakati akiweka jiwe la msingi la ukarabati wa kituo cha Afya Koromije na kukagua hali ya utoaji Huduma za Afya katika Hospitali ya Wilaya ya Misungwi, Mwanza.

“Haina maana ya kuwa na majengo makubwa na mazuri ya Vituo vya Afya kama hakuna vifaa vinavyohitajika, huku Wananchi wanaendelea kupata tabu,” alisema Waziri Ummy.

Aidha, Waziri Ummy amewahasa wazazi na wananchi wote kwa ujumla kutodharau huduma za chanjo, hivyo kuwahimiza Wananchi wote kuwapeleka katika vituo vyakutolea chanjo watoto waliofika umri wa kupata chanjo

“Kifafa, kifaduro, donda koo, surua, hayapo siku hizi kwa sababu ya chanjo, kwa hiyo tusije tukadharau chanjo, tuhakikishe kila mtoto mwenye umri wakupata chanjo , akapate chanjo,” alisema Waziri Ummy Mwalimu.

Aidha, Waziri Ummy amewataka wananchi wa Misungwi kuhakikisha wanasafisha mazingira, na kutumia vyandarua vyenye dawa ili kuepuka kupata ugonjwa wa Malaria ambao umeendelea kuwa hatari nchini hasa kwa watoto wenye umri chini ya miaka 5 na Wanawake Wajawazito.

“Ugonjwa wa Malaria umepungua kutoka asilimia 37 hadi 27, kwahiyo niendelee kuwahimiza Wananchi wa Misungwi, kwanza kuhakikisha wanafukia vidimbwi vya maji, kusafisha mazingira na kulala kwenye vyandarua vyenye dawa,” alisema Waziri Ummy.

Waziri Ummy aliendelea kusisitiza kuwa sio kila homa ni Malaria, hivyo kuwataka Wananchi kutotumia dawa bila kwenda kupata vipimo katika Kituo cha kutolea Huduma za Afya na kuthibitishwa kuwa una Malaria.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dk. Rutha Thomas alisema kuwa Mkoa wa Mwanza unaishukuru Serikali kwa kuwapatia jumla ya Sh. 2 bilioni zitakazotumika katika ujenzi wa Hospitali 2 za Hamashauri za Ilemela na Bushosa.

Mwisho.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Sabaya afutiwa kesi, ruksa kugombea uongozi

Spread the loveMwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP leo Ijumaa amefuta rufaa...

AfyaHabari Mchanganyiko

200 wapimwa afya na GGML katika maonesho ya OSHA

Spread the loveZAIDI ya watu 200 jijini Arusha wamejitokeza kupimwa afya na...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kwafukuta kisa chaguzi, Lissu aibua tuhuma nzito

Spread the loveCHAGUZI za kusaka viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo...

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga “HIDAYA” chaendelea kuimarika, wananchi wapewa tahadhari

Spread the loveMAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kutoa taarifa...

error: Content is protected !!