February 26, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Vigogo Chadema wagonga mwamba mahakamani

Spread the love

MAHAKAMA Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, imekubaliana na maombi ya Jamhuri ya kughairisha usikilizaji wa rufaa ya mwenyekiti wa Chadema, Freman Mbowe na Mbunge wa Tarime, Ester Matiko. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Maamuzi hayo yametolewa muda mfupi uliopita mahakamani hapo na Jaji Sam Runyamika anayesikiliza shauri hilo.

Kabla ya kufikia maamuzi hayo, Jaji Runyamika alitoa nusu saa kuamua, iwapo maombi ya Mbowe na Matiko ya kupewa dhamana yaendelee kusikilizwa ama yasubiri maamuzi ya rufaa.

Serikali iliwasilishwa mahakamani muda mfupi kupinga usikilizaji wa shauri hilo hadi rufaa yao itakaposikilizwa.

error: Content is protected !!