Saturday , 4 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Halima Mdee, wanachama wa Chadema wakamatwa jioni hii
Habari za SiasaTangulizi

Halima Mdee, wanachama wa Chadema wakamatwa jioni hii

Spread the love

TAARIFA KWA UMMA

Mwenyekiti wa BAWACHA Taifa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama, Halima Mdee (Mb) pamoja na viongozi wengine, wanachama na wapenzi wa CHADEMA Jimbo la Kawe takriban 13, wamekamatwa na wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Kituo cha Polisi Kawe.

Hadi sasa jeshi hilo halijatoa taarifa rasmi kueleza sababu ya kumshikilia mbunge huyo pamoja na wananchi wake baada ya kuwakamata maeneo ya Tanganyika Parkers, Kawe, jijini Dar es Salaam.

Awali, Mdee ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Kawe, alisimamishwa na wananchi alipopita maeneo hayo, wakitaka kumpatia kero zao.

Baada ya kusikiliza malalamiko ya wapiga kura wake na kuondoka, inadaiwa polisi walifika eneo hilo na kuanza kuwakamata walioonekana kuwa na sare za CHADEMA.

Alipopata taarifa hizo, Mdee alilazimika kurudi ambapo polisi hao wakiongozwa na Askari Polisi mwenye cheo cha Inspekta walimuamuru Mdee na viongozi hao kuelekea kituoni.

Hadi sasa viongozi hao bado wako kituoni hapo.

Tumaini Makene.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano CHADEMA.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Sabaya afutiwa kesi, ruksa kugombea uongozi

Spread the loveMwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP leo Ijumaa amefuta rufaa...

Habari za Siasa

Serikali yasaka bilioni 3 kujenga daraja Mto Mpiji

Spread the loveSerikali imesema inaendelea na juhudi za kutafuta fedha kiasi cha...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kwafukuta kisa chaguzi, Lissu aibua tuhuma nzito

Spread the loveCHAGUZI za kusaka viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo...

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga “HIDAYA” chaendelea kuimarika, wananchi wapewa tahadhari

Spread the loveMAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kutoa taarifa...

error: Content is protected !!