MABINGWA wa Ligi Kuu Tanzani Bara, Simba wanatarajia kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Asante Kotoko kutoka Ghana katika maadhimisho ya siku ya Simba (Simba Day) yanayotarajia kufanyika katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam 8 Agosti 2018.
Akiongea na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa Hotel ya Serena, Mkuu wa idara ya Habari ndani ya klabu hiyo Haji Manara amesema kuwa hapo awali kulikuwa na taarifa ya kuwa watacheza na AFC Leopard kutoka Kenya lakini taarifa hiyo sio sahihi bali watakipiga na mabingwa hao wa Ligi Kuu ya Ghana.
“Taarifa ambazo zilikuwa zikienea kwamba tutacheza dhidi ya AFC Leopard kutoka Kenya si za kweli na tutacheza na hiyo ambayo tumeitaja,” amesema Manara.
Licha ya hayo Msemaji huyo aliongezea ya kuwa katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya Simba day ndani ya wiki hii wanatarajia kufanya shughuli mbali mbali za kijamii.
Simba ambayo kwa sasa imeweka kambi nchini Uturuki kwa ajiri ya kujiandaa na msimu mpya kwa michuano ya ligi kuu na kombe la klabu bingwa barani Afrika ambao watakuwa wanawakilisha nchi.
Leave a comment