Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Tanzania kujitangaza kibiashara soko la EAC
Habari Mchanganyiko

Tanzania kujitangaza kibiashara soko la EAC

Pindi Chana, Balozi wa Tanzania nchini Kenya
Spread the love

BALOZI wa Tanzania nchini Kenya, Pindi Chana imeiomba sekta binafsi kujitokeza ili kushiriki maadimisho ya biashara hapa nchini yatakayofanyika Aprili 26 mwaka huu kwa lengo la kukuza uchumi wa viwanda. Anaripoti Angel Willium … (endelea).

Maadhimisho hayo yameandaliwa kwa ushirikiano wa wizara ya mambo ya nje nchini Kenya na wizara ya viwanda na biashara hapa nchini.

Akizungumza na waandishi wa Balozi Chana amesema serikali imeandaa maadhimisho ya kibiashara, ili kuzitangaza bidhaa za hapa nchini katika soko la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

“Soko kubwa kwa EAC lipo nchini hivyo bidhaa zetu tunatakiwa kupeleka katika nchi hiyo ambayo ni majirani zetu, wafanyabiashara wa viwandani na wajasiriamali wanatakiwa kuzitangaza bidhaa mbalimbali kama vitenge, sabuni, maji ya kunywa,dawa za mswaki,” amesema

“Tunatarajia kufanya wiki maalumu ya kuzitangaza bidhaa za Tanzania, ili ziweze kufika nchini ya Kenya hivyo nachukua nafasi hii kuwa karibisha wafanyabiashara wa viwanda na wajasiria mali wajitokeze katika siku hivyo,”amesma chana.

Aidha, Mkurugenzi wa kampuni ya Lake Group, Khaled Hassani amesema, Kenya ni nchi ambayo ina biashara nyingi na wanahakikisha wanazuia biashara yoyote kutoka nje kuingia nchini mwao.

Amesema kampuni yake ilikutana na vipingamizi vingi ilipotaka kuingia nchini Kenya na kwamba kwa sasa wanashika nafasi ya pili mauzo ya gesi.

Maadhimisho yatakuwa yanafanyika kila mwaka katika sikukuu ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!