Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Shirika la Posta labadili nembo yake
Habari Mchanganyiko

Shirika la Posta labadili nembo yake

Spread the love

SHIRIKA la Posta Tanzania, limezindua nembo mpya ya shirika hilo baada ya ile ya zamani kukaa zaidi ya miaka 24 hadi kufika leo, anaandika Nasra Abdallah.

Hafla hiyo pia iliendana na uzinduzi wa  mabasi  yatakayotumika kusafirishia abiria na vifurushi kama njia mojawapo ya kuifanya kazi hiyo kwa usalama zaidi.

Akizungumza katika uzinduzi huo ulifanywa leo jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri Wa wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa amesema nembo hiyo ni moja ya utekelezaji wa mageuzi yanayofanywa kwa sasa na shirika hilo.

Kwandikwa amesema mageuzi hayo ni pamoja na uanzishwaji wa kampuni tanzu nne sambamba na mabadiliko ya muundo na mifumo ya kiutendaji itakayosaidia katika kusimamia na kuendesha miradi itakayoanzishwa.

“Ni hivi karibuni mlizindua huduma ya ya ‘Posta Mlangoni’, hicho pekee ni kielelezo sahihi cha jitihada hizi na matarajio yangu kuwa huduma mpya zitasimamiwa kikamilifu ili ziweze kufikia malengo yaliyokusudiwa,” amesema Waziri huyo.

Kuhusu mabasi matatu yaliyozinduliwa, Postamasta Mkuu, Hassan Mwang’ombe amesema wameyapata kutoka Umoja wa Posta Duniani baada ya kuridhishwa na utendaji kazi wa shirika hilo ambayo thamani yake yote ikiwemo Lori la tani 10 ni sh. 757 milioni.

Mwang’ombe amesema kwa kuanzia mabasi hayo yatakuwa yakibeba barua, vifurushi na abiria katika baadhi ya njia zenye shida ya usafiri ikiwemo Makambako (Njombe)  na Masasi (Mtwara).

“Pamoja na kwamba lengo kuu la kupeleka mabasi hayo  maeneo hayo ni kusafirisha barua na vifurushi ili kuongeza kasi ya usalama, ni wazi kuwa gharama za uendeshaji zitafidiwa na tozo ya nauli watakayotozwa abiria watakaotumia mabasi hayo na kuyafanya yaweze kumudu gharama za uendeshaji,” amesema Postamasta huyo.

Awali Mwenyekiti wa Bodi  wa Shirika hilo, Kanali Mstaafu Haroun Kondo, amesema mpaka walipofikia sasa haikuwa kazi rahisi na imetokana na ushirikiano mkubwa uliopo Kati ya wafanyakazi, menejimenti na Bodi.

Kanali Kondo amesema pamoja na mambo mengine shirika litaendelea kuboresha matawi take ya ofisi za posta zilizoko mikoani na wilayani ili ziweze kutoa huduma bora zaidi na kuchangia uchumi na jamii kwa ujumla.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyakazi waidai STAMICO mishahara ya bilioni 1

Spread the loveWALIOKUWA wafanyakazi wa mgodi wa Shirika la Madini la Taifa...

AfyaHabari Mchanganyiko

200 wapimwa afya na GGML katika maonesho ya OSHA

Spread the loveZAIDI ya watu 200 jijini Arusha wamejitokeza kupimwa afya na...

Habari Mchanganyiko

Mfanyakazi CRDB atoa sababu za kubambikiwa kesi, hukumu Mei 30

Spread the love  MFANYAKAZI wa Benki ya CRDB, Ibrahim Masahi (40) ameieleza...

Habari Mchanganyiko

Waziri Ummy atangaza Tanzania kuwa kitovu cha utalii tiba

Spread the loveSERIKALI imesema imedhamiria kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha matibabu ya...

error: Content is protected !!