March 8, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Polisi wainua mikono kupigwa risasi Lissu

Tundu Lissu, Mwanasheria Mkuu wa Chadema

Spread the love

JESHI  la Polisi limefunga mwaka huku likishindwa kutoa majibu kuhusu watu waliohusika kumpiga risasi zaidi ya 38, Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema), anaandika Angel Willium.

Mkurugezi wa Upelezi wa Makosa ya Jinai (DCI),  Robert Baoz amesema, mpaka sasa wanalichukulia kwa ukubwa suala hilo la Lissu kupigwa risasi, lakini limeshindwa kusema kama limekamata watuhumiwa wowote mpaka sasa.

Lissu alipigwa risasi mwezi Septemba mwaka huu mjini Dodoma na kukimbizwa hospitali nchini Kenya ambapo anaendelea kupatiwa matibabu mpaka sasa.

Kwa upande mwingine Baoz amesema walipokea taarifa ya mwandishi wa habari wa Mwananchi kupotea  na kwamba wanachukua kila hatua kuhusu suala hilo.

Akitoa takwimu za uhalifu nchini, Boaz amesema kulikuwa na makosa mbalimbali ya uhalifu kwa mwaka 2017 huku akisema suala la ubakaji kwa watu wazima limeongoza kuliko makosa yote likifuatiwa na kunajisi kwa watoto wadogo.

Matukio mengine ya uhalifu yaliyotikisa kwa mwaka huu ni kutupa watoto, wizi wa watoto, kulawiti pamoja na usafirishaji wa binadamu.

Amesema makosa hayo yamekuwa na idadi kubwa kuliko makosa mengine yaliyotokea kati ya January hadi Novemba 2016 ikilinganisha na mwaka huu.

Amefafanua kuwa mwaka jana  yalikuwa 11,513 na mwaka huu ni 11,620  ambayo yaliripotiwa sawa na ongezeko la makosa 107 sawa na asilimia 0.9.

Baoz amesema makosa yameongezeka kwa upande wa ubakaji na kunajinsi ambapo kwa mwaka 2016 yalikuwa  6,985, ikilinganishwa na  7,460  mwaka huu.

Amesema hilo ni ongezeko la  makosa 478 sawa na asilimia 6.8 wakati makosa ya kunajinsi yalikuwa 16 kwa mwaka jana  na 25 ya mwaka huu sawa na ongezeko la makosa tisa ambayo ni asilimia 56.3.

error: Content is protected !!