Sunday , 28 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Sumaye, Lowassa watajwa sakata la madini bungeni
Habari za SiasaTangulizi

Sumaye, Lowassa watajwa sakata la madini bungeni

Mawaziri Wakuu Wastaafu, Frederick Sumaye (kushoto) na Edward Lowassa walipokuwa katika kampeni za Chadema
Spread the love

WAKATI wabunge wa upinzani wakishinikiza marais waliopitisha mikataba mibovu kuhojiwa, Job Ndugai, Spika wa Bunge la Tanzania amewaibua Mawaziri wastaafu Edward Lowassa na Fredrick Sumaye, anaandika Hamisi Mguta.

Ndugai amesema kuwa wabunge wa Chadema wanaoshinikiza marais wastaafu wahojiwe wakumbuke kuwa chama hicho pia kina mawaziri wakuu wastaafu wawili ambao watahusika.

“Mabadiliko mnayoyataka yakipitishwa na viongozi mlionao wakikamatwa msije mkalalamika tena,” amesema Ndugai.

Mawaziri wastaafu waliopo Chadema ni Edward Lowassa aliyekuwa Waziri Mkuu wa Awamu ya Nne na Frederick Sumaye, Waziri Mkuu Mstaafu wa Awamu ya Tatu, ambao walihamia chama hicho wakitokea CCM mwishoni mwa mwaka 2015.

Katika mchango wake bungeni, Peter Lijualikali amesema, haiwezekani watendaji wa serikali wakapitisha mikataba mibovu ya madini bila ridhaa ya rais hivyo marais wastaafu wanatakiwa kuhojiwa.

“Haiwezekani Mzee wangu Chenge (Andrew) na Karamagi (Nazir) walipitisha mikataba hiyo bila Rais aliyekuwapo kufahamu. Kinga ya Rais kushtakiwa iondolewe ili wahojiwe,” amesema Lijualikali.

Hoja hiyo ya Lijualikali inafanana na ya John Heche (Chadema), Mbunge wa Tarime
Vijijini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

Habari za Siasa

Sauti ya Watanzania waeleza sababu za kuiunga mkono Chadema

Spread the love  KIKUNDI kinachojipambanua katika kupigania rasilimali na uhuru wa nchi,...

Habari MchanganyikoTangulizi

Jacob, Malisa waachiwa kwa masharti

Spread the love  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

error: Content is protected !!