Friday , 26 April 2024
Home Habari Mchanganyiko 32 wahitimisha promosheni Bonge la Mpango ya NMB
Habari Mchanganyiko

32 wahitimisha promosheni Bonge la Mpango ya NMB

Spread the love

 

KAMPENI ya Benki ya NMB ya kuwahamasisha wateja wake kuweka akiba ya Bonge la Mpango awamu ya pili imeimehitimishwa kwa washindi 32 kujinyakulia zawadi zenye thamani ya Sh.100 milioni. Anaripoti Mwandishi Wetu, Pwani … (endelea).

Miongoni mwa washindi wa droo ya mwisho ya promosheni hiyo kabambe walikuwa ni wateja 22 wa NMB walioshinda pikipiki za miguu mitatu aina ya Skymark ambazo bei ya kila moja ni Sh.4.5 milioni.

Pia, katika kuhitimisha shindano hilo la wiki 12 lililoanza Oktoba 2021, washindi 10 walishinda Sh.100,000 kila mmoja.

Akizungumza wakati wa droo ya mwisho iliyofanyika kwenye Tawi la NMB la Bagamoyo mkoani Pwani, mwishoni mwa wiki iliyopita, fisa Uhusiano Amana za Wateja wa benki hiyo, Monica Job, alisema kampeni hiyo imefanyika kwa mafanikio na ufanisi mkubwa.

Aidha, kiongozi huyo alitabainisha promosheni hiyo imenufaisha wateja zaidi ya 170 na kuwachagiza wengine kuchangamkia fursa kama hizo na huduma zinazoendelea kubuniwa na kutolewa na Benki ya NMB.

Lengo la “Bonge la Mpango II” kama ilivyokuwa kwa mtangulizi wake ilikuwa kurejesha fadhila kwa wateja waaminifu na kuwahamasisha kujenga utamaduni wa kuweka akiba.

Kwenye droo ya mwisho iliyosimamiwa na Afisa wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), Pendo Mfuru, washindi 17 walitwaa pikipiki za fainali, watatu wakijibebea pikipiki za mwisho wa mwezi na wawili walishinda pikipiki za droo ya wiki.

“Hii imekuwa ni kampeni iliyofanyika kwa mafanikio makubwa, huku ikiwanufaisha wateja wetu wengi sana,” amesema

“Tuliitumia sio tu kuhamasisha utamaduni chanya wakuweka akiba, bali pia kama sehemu ya utamaduni wa NMB wa kugawana faida na wateja wake na kurudisha kwa jamii. Tunashukuru kwa sababu malengo haya yote yamefanikiwa kwa asilimia kubwa,” amesema Monica.

Kwa upande wake, Mfuru aliipongeza NMB kwa kampeni hiyo akisema ilifanyika kwa kufuata sheria, vigezo, masharti na taratibu zinazosisitizwa na GBT na kwamba benki hiyo ilizingatia hayo yote katika kila droo ya Bonge la Mpango II.

Katika promosheni hiyo, kila wiki washindi 10 walijishindia fedha taslimu na wawili pikipiki za Skymark, huku droo za mwisho wa mwezi zikiwazawadia washindi watatu pikipiki hizo za kisasa.

Jumla ya Skymark 50 zilinyakuliwa kwenye kampenihiyo iliyokuwa na zawadi zenye thamani ya zaidi ya Sh.246 milioni ambazo washindi wake walitoka sehemu mbalimbali nchini.

Washindi walioshinda pikipiki za droo ya mwezi Desemba na matawi yao kwenye mabano ni: Emmanuel Kavishe (Zanzibar), Mbila Salum (Mafinga) na Albert Mhehe (Mkwawa).

Waliojinyakulia pikipiki 17 za droo ya fainali ni: Frank Mgeni (Ngaramtoni), Bundala Gwanona (Geita), Mary Martine (Kenyatta Road), Misoji Joseph (Kenyatta Road), Martha Makorere (Tarime), Ambakisye Kyomo(Kaitaba), Paschal Kaloli (Geita) na Herieth Alphonce (Babati).

Wengine ni Elineema Ezekiel (Babati), Khamis Abbas (Sikonge), Hamalos Kahindi (Nzega), Mathias Lusendamila (Manonga), Clement William (Wami), Michael Kabume (Mvomero), Glory Mwalongo (Mvomero), Marc Constantine (Wami) na Aziza Nzoto (Mvomero).

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!