January 15, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Zitto, Mdee washinda tuzo ya mwanasiasa bora mtandaoni

Aliyekuwa Mbunge wa Kawe kupitia Chadema, Halima Mdee akitafakari jambo bungeni

Spread the love

KIONGOZI wa Chama Cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe na aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la Chadema (Bawacha), Halima Mdee,  wameshinda tuzo za Watu, Taasisi na Chapa, zinazoongoza mtandaoni (Tanzania Digital Awards), kwenye kipengele cha Mwanasiasa bora. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Wanasiasa hao wameshinda tuzo hizo baada ya kupata kura nyingi, katika kipengele cha mwanasiasa bora mtandaoni.

Katika tuzo hizo zilizotolewa jana tarehe 25 Desemba 2020, Zitto ameshinda kipengele cha mwanasiasa bora wa kiume mtandaoni kwa mwaka 2020, huku Mdee akishinda kipengele cha mwanasiasa bora wa kike.

Kwenye kipengele cha mwanasiasa bora wa kiume, Zitto alichuana na aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Godbless Lema. Aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamis Kigwangalla.

Na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole. Pamoja na Mbunge wa Bumbuli kupitia chama hicho, January Makamba.

Mdee alichuana na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani, Jokate Mwegelo. aliyekuwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza. Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Ummy Mwalimu.

Na, aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, anayesimamia masuala ya uwekezaji, Angellah Kairuki.

Katika tuzo hiyo, wananchi walipiga kura kuchagua mwanasiasa bora katika kutumia mitandao ya kijamii kuongoza wananchi kwenye kuleta maendeleo.

Tuzo hizo zinalenga kutambua mchango wa watu na taasisi ambazo zinatumia kifanisi na kwa ubunifu majukwaa na teknolojia za kidigitali kuhamasisha na kuchagiza maendeleo ya kudumu katika mitandao na jamii.

error: Content is protected !!