Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Zitto, Maalim Seif wapiga kambi Segerea
Habari za Siasa

Zitto, Maalim Seif wapiga kambi Segerea

Spread the love

ZITTO Kabwe, Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo na Maalim Seif Sharif Hamad, mshauri wa chama hicho leo tarehe 28 Julai 2019, wamelivaa Jimbo la Segerea, jijini Dar es Salaam. Anaripoti Hamis Mguta … (endelea).

Viongozi hao wawili tangu asubuhi ya leo, wamefika kwenye jimbo hilo wakifanya harakati mbalimbali za chama hicho ikiwa ni pamoja na kufungua matawi 10, wakieleza kuwa ni maandalizi kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu.

Maalim Seif na Zitto wamebeba ujumbe tofauti kwenye ufunguzi wa atawi hayo. Wakati wakifungua matawi hayo Vingunguti Maalim Seif amewataka vijana kuwa imara kutetea demokrasia nchini.

Maalim Seif ambaye alikuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), na kuachana na chama hicho kutokana na mgogoro wa ndani, amesema Taifa linawategemea vijana kwenye mabadiliko.

Amewaeleza vijana kuwa wanapaswa kufikiria maisha yao ya mbele kwa kusimamia vema demokrasia, na kuwa ujasiri wao ndio njia pekee ya kusimamia demokrasia waitakayo nchini.

“Mnapswa kuwa imara na majasiri kusimamia demokrasia,” amesema Maalim Seif akiongeza kuwa “ACT Wazalendo ndiyo kinachobeba mnayoyahitaji. Malengo yetu ni kuongoza serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, matumaini yetu yote ni kwenu vijana.”

 Kwenye ziara hiyo Zitto ametoa wiko kwa serikali kuhakikisha kuwa uchaguzi wa serikali za mitaa unakuwa huru na haki. Ameelekeza rai yake kwa Suleiman Jafo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) kusimamia haki kwenye uchaguzi huo.

Zitto amewataka wananchi kuwa tayari kwa mabadiliko yatayoletwa kupitia chama hicho, na kuwa wanapaswa kujiandaa kuyapokea.

Zitto na Maalim Seif wametembea mtaa kwa mtaa kufungua matawi kwenye jimbo hilo huku wakiwataka wananchi kuinuka na kuikataa CCM.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!