Friday , 9 June 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Usawa na utu havitoshi, lazima haki iwepo – Butiku
Habari za Siasa

Usawa na utu havitoshi, lazima haki iwepo – Butiku

Spread the love

JOSEPH Butiku, Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku amewataka wanasiasa nchini kusimamia haki kwa kuwa utu na usawa pekee havitoshi. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Akizungumza kwenye mkutano wa Chama cha NCCR-Mageuzi, uliofanyika kwa lengo la kuchagua viongozi wapya wa chama hicho tarehe 27 katika ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dae rs Salaam, amesema inahitajika unyenyekevu kusimamia amani.

“Usawa na utu hautoshi, lazima kuwe na haki maana kila mtu anastahili haki, msingi huo ndio unatawala vyama vyetu vyote,” amesema Butiku akisistiza kwamba “tukifanya hayo, tutapata amani.”

Mwanasiasa huyo mkongwe nchini, amesema vyama vinapaswa kuwa na utaratibu wa kujifunza kutoka kwenye vyama vingine, na kwamba jambo hilo linaweza kusaidia kuendeleza Amani iliyopo sasa.

 “Ninashukuru mmepata nafasi ya kutuita hapa na ninawaombea muendelee hivyo, Mbatia huwa ninakuangalia huwa unasema mambo mengi ya busara hivyo ongoza chama hiki kiwe cha busara na kisaidiane na chama tawala nacho kijifunze,” amesema.

“Mimi ninajifunza kwenu miaka yangu 81 ninawafundisha na kujifunza pia, ninyi vyama mlivyotangulia na vilivyozaliwa jengeni uwezo kwa kujifunza miongoni mwenu, CCM mjifunze kwa vingine na ninyi mjifunze kutoka kwao pia na mfanye hivyo kwa unyenyekevu,” amesema.

Aidha amesisitiza vijana kuwa na utu kwakua ndio msingi wa Taifa la Tanzania ambapo amesema iwapo kutakuwa na utu, usawa na na haki nchi itakuwa na amani.

“Ninawakumbusha vijana taifa hili wakati linaasisiwa msingi wake ulikua ni utu na usawa wa utu ukikataa hilo maana yake unakataa utu kwasababu mwenzako nae anaweza akakukataa,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Lussu: Mkataba wa DP bandarini si wa miaka 100

Spread the loveMAKAMU Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, amesema hakuna ukweli wowote...

Habari za SiasaTangulizi

Maulid Mtulia: Kutoka ubunge hadi U-DAS

Spread the love ALIYEKUWA mbunge wa Kinondoni, kupitia vyama vya The Civil...

Habari za Siasa

Lusinde: CCM hatuliachii ng’o jimbo la Moshi Mjini

Spread the loveMJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC), Livingston...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar: Bakharesa hajavamia shamba letu

Spread the love  IKULU Visiwani Zanzibar, imeeleza kuwa eneo la kiwanda cha...

error: Content is protected !!