September 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mbatia apewa miaka mitano NCCR-Mageuzi

Spread the love

JAMES Mbatia, amechaguliwa tena kuwa Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi huku Angelina John, akichaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti Bara na Ambar Hamis ameukwaa umakamu mwenyekiti visiwani Zanzibar. Anaripoti Faki Sosi…(endelea).

Florian Mbeo, mkuu wa oganaizesheni na utawala wa chama hicho amesema, Mbatia na timu yake itaongoza chama hicho kwa miaka mitano ijayo kwa mujibu wa katiba yao.

Mkutano wa chama hicho leo tarehe 28 Julai 2019 pia umechagua wajumbe wa halmashauri kuu ambapo Mbeo amesema, kwa mujibu wa katiba yao, anapotokea mgombea mmoja kwenye nafasi, basi hupiga kura za ndio ama hapana.

Akifafanua namna Mbatia alivyopita na kuendelea kuongoza chama hicho amesema, katika nafasi ya uenyekiti alijitokeza yeye (Mbatia) peke yake ambapo alipigiwa kura za ndio 201 huku tisa zikimkataa.

“Kwa mujibu wa matokeo hayo, Mhe Mbatia atakuwa mwenyekiti wetu kwa miaka mitango mingine ijayo,” amesema Mbeo na kuongeza “viongozi wengine wanaendelea kuchaguliwa.”

error: Content is protected !!